Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akiwapokea makada wa Chadema jimbo la Iringa mjini walioamua kuachana na Chadema na kujiunga na CCM
Maandamano ya boda boda na magari katika kuhitimisha mbio za Bendera ya CCM mkoa wa Iringa
Wananchi wa maeneo ya Miyomboni eneo la mashine tatu wakishuhudia msafara wa Bendera ya CCM ukipita eneo hilo
Makada wa Chadema wakisalimisha kadi zao kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Bi Jesca Msambatavangu
Umati mkubwa wa wananchi waliojipanga barabarani wakati wa msafara wa bendera ukipita
Msafara wa bendera katika manispaa ya Iringa
Wananchi wakiwa katika mkutano wa kilele cha mbio za bendera mkoa wa Iringa
Vijana walioshiriki kukimbiza bendera ya CCM mkoa wa Iringa
Kada wa Chadema katikati Violeth Mwakisyala akiwa ameungana na wana CCM kuweka alama ya dole baada ya kujivua Chadema na kujiunga CCM
| Kada wa CCM Bw Julio Elieza kushoto akisoma maandishi ya CHANA GWANDA NA GAMBA NA VAA UZALENDO mara baada ya kujiunga na CCM akitokea Chadema |
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa akimkaribisha CCM Bi Violeth baada ya kujiengua Chadema
Makada na wapiganaji wa Chadema waliojiunga na CCM
Kiapo cha utii kwa waliojiunga na CCM kutoka vyama mbali mbaliKiongozi mkuu wa mbio za bendera Alli Simba akijiandaa kumkabidhi bendera diwani wa kata ya Makorongoni Bw Thadeus Tenga ili akabidhi kwa mwenyekiti wa CCM mkoa
Tenga akijiandaa kupokea bendera toka kwa Simba
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kulia akipokea bendera toka kwa diwani wa kata ya makorongoni na kiongozi wa mbio hizo
Na Francis Godwin Blog
MBUNGE wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amerushiwa makombora na baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao juzi walitimkia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Makombora
hayo yalirushwa katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa, wakati CCM
Mkoa wa Iringa ikihitimisha mbio zake za bendera ya CCM.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu alisema lengo la mbio za
bendera ya CCM ni kuhamasisha amani na utulivu nchini.
Malengo
mengine ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho unaofanywa na
serikali, kuhamsisha vijana kujiajiri na kuwashukuru watanzania kwa
kuendelea kuinga mkono CCM.
Katibu
Uenezi na Itikadi Mkoa wa Iringa, Dk Yahaya Msigwa alisema jumla ya
wanachama 120 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani kikiwemo Chadema
wamerejea CCM kupitia mbio hizo.
Baadhi
ya wanachama wa Chadema waliokabidhiwa kadi zao kwenye hitimisho la
mbio hizo zilizoanza miezi miwili iliyopota ni pamoja na Ibrahim Mmasi
na Vaileti Mwakisyala.
Akirusha makombora kwa Mchungaji Msigwa, Mmasi alisema ni kiongozi asiyeambilika huku akimtuhumu kwamba ni mroho wa madaraka .
Mmasi
alisema wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, Mchungaji Msigwa
aliwatuhumu baadhi ya viongozi akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Iringa Mjini Monica Mbega (CCM) kwa kuwa na vyeo vingi vya kisiasa hali
iliyosababisha ashindwe kutekeleza wajibu wake kwa wananchi.
“Wananchi
walimsikia Mchungaji Msigwa na kumpa ubunge, lakini baada ya kupata
nafasi hiyo anazidi kujilimbikizia vyeo hali inayofinya demokrasia ndani
ya chama,” alisema.
Akivitaja
baadhi ya vyeo vya mbunge huyo, Mmasi alisema mbali ya kuwa mbunge,
Mchungaji huyo ni diwani, mwenyekiti wa chama hicho wilaya, mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chadema na waziri kivuli.
Alisema
hali ya kisiasa ndani ya chama hicho wilayani hapa na mkoani kwa ujumla
sio nzuri kwa kuwa hakuna demokrasia ya kukosoa na kukosolewa.
“Kuna udikteta wa mawazo, watu wakisema ukweli wanachukiwa, mambo hayako shwari hata kidogo,” alisema.
Alisema
kuna viongozi ambao hawapikiki chungu kimoja na mchungaji Msigwa,
hawasalimiani, hawaaminiani kwa kile kinachoelezwa kwamba hapendi
kukosolewa.
Huku
akishangiliwa na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, Mmasi
alisema kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao, Chadema mjini Iringa itakuwa
imesambaratika.
“Uchaguzi
ndani ya chama hicho umekaribia, waliopo na tuliokuwepo tunajua
kinachoendela, hali sio nzuri kwasababu wanachama walio wengi wanataka
mabadiliko, hali hiyo haitawaacha salama,” alisema.
huku
wanachama zaidi ya 200 wapya wakijiunga na chama hicho huku
baada ya makada wa chama cha Demokrsani na maendeleo (CHADEMA)
wakijiengua katika chama hicho na kujiunga na CCM.
Makada hao wa Chadema wameeleza kufurahishwa na utendaji kazi wa serikali ya CCM na kuchukizwa kile walichodai ni ubabaishaji wa Chadema katika ngani ya jimbo , mkoa na Taifa kwa madai kuwa vitendo vya kifisadi ndani ya Chadema ni moja ya sababu ya wao kujiengua.
Makada hao wakitumia muda mwingi kushambulia mbunge wa jimbo la Iringa mjini na diwani wa Mvinjeni na viongozi wa Chadema taifa walisema kuwa wamechoshwa na porojo za viongozi hao.
Pia vijana hao walisema kuwa wamekuwa wakipokea vitisho mbali mbali kutoka kwa viongozi na makada wa Chadema pale wanapotaka kuhamia CCM
Makada hao wa Chadema wameeleza kufurahishwa na utendaji kazi wa serikali ya CCM na kuchukizwa kile walichodai ni ubabaishaji wa Chadema katika ngani ya jimbo , mkoa na Taifa kwa madai kuwa vitendo vya kifisadi ndani ya Chadema ni moja ya sababu ya wao kujiengua.
Makada hao wakitumia muda mwingi kushambulia mbunge wa jimbo la Iringa mjini na diwani wa Mvinjeni na viongozi wa Chadema taifa walisema kuwa wamechoshwa na porojo za viongozi hao.
Pia vijana hao walisema kuwa wamekuwa wakipokea vitisho mbali mbali kutoka kwa viongozi na makada wa Chadema pale wanapotaka kuhamia CCM
Msambatgavangu
alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa haitawavumilia viongozi wa
serikali ambao watashindwa kutekeleza majukumu yao .
Huku ikiwatoa hofu vijana waliopo upinzani ambao wanataka kurudi CCM kuwa wana uhuru wa kwenda chama chochote cha siasa.
Huku ikiwatoa hofu vijana waliopo upinzani ambao wanataka kurudi CCM kuwa wana uhuru wa kwenda chama chochote cha siasa.
Kwa
kupitia mbio hizo za bendera Msambatavangu alisema jumla ya wanachama
wapya 4,000 wamepatikana katika wilaya zote za mkoa wa Iringa, na
wanachama zaidi ya 1,000 wamejiunga na jumuiya mbalimbali za CCM

0 comments:
Post a Comment