MKONGWE
wa muziki wa dansi Kassim Mapili amethibisha kushiriki Tamasha la
Gurumo 53 litakalofanyika Jumamosi ya tarehe 14 mwezi Disemba mwaka huu.
Mapili
amesema si yeye tu, balipia ataratibu mpango mzima wa kuhakikisha
wakongwe wote wa muziki wa dansi wanashiriki tamasha hilo bure bila
malipo yoyote.
Tamasha
hilo ambalo ni mahsusi kwaajili ya kumuaga mwimbaji mkongwe Muhidi
Maalim Gurumo litafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya TCC
Club Chang’ombe.
Mratibu
wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Mapili ameamua kubeba jukumu la
kuandaa wakongwe ambao ambao watatengeneza wimbo maalum wa kumuaga
Gurumo utakaosikika kwa mara ya kwanza TCC Club Disemba 14.
Baadhi
ya wakongwe wengine waliothibitsha kushiriki Tamasha la Gurumo 53 ni
pamoja Komandoo Hamza Kalala, Tshimanga Kalala Assossa na Waziri Ali.
Gurumo anaagwa kufuatia kutangaza kwake kuachana rasmi na muziki wa jukwaani baada ya kudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 53.
Bendi
za Twanga Pepeta, Msondo Ngoma na wanamuziki kibao waliowahi kung’ara
na Sikinde ni sehemu ya wasanii watakaosindikiza tamasha hilo
linalosubiriwa kwa hamu.
Hadi
kustaafu kwake Gurumo aliyezitumikia pia bendi za Kilimanjaro
Chacha,Rufiji Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na OSS – Ndekule, alikuwa ni
kiongozi na mmoja wa wamiliki wa Msondo Ngoma.
Wasanii
waliowahi kuitumikia Sikinde ambao watakuwepo kumsindikiza Gurumo ni
pamoja na Cosmas Chidumule, Abdallah Gama, Hussein Jumbe, Mashaka
Shaaban, Kalamazoo, Henry Mkanyia na Karama Legesu. Wengine ni Ali
Yahaya na Boniface Kachale, Benno Villa Anton, na Ibrahim Mwinchande.
Hata
hivyo, licha ya wasanii hao waliowahi kuitumikia Sikinde kuwemo kwenye
tamasha hilo, bendi ya Mlimani Park “Sikinde Ngoma ya Ukae” haitashirki
katika Gurumo 53 kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wao.
Mbizo
amesema Mlimani Park ina mkataba unaowabana kufanya onyesho lolote
litakalowakutanisha na Msondo hadi baada ya sikukuu ya Krismasi (Disemba
25, 2013).
Juma
Mbizo amesema licha ya Sikinde kutoshiriki tamasha hilo lakini nyimbo
zote zilizotamba ndani ya bendi hiyo ambazo zilitungwa na Gurumo,
zitarindima TCC Club kwa ubora ule ule.
“Wanamuziki
wengi waliofanya kazi na Gurumo katika Sikinde enzi hizo, hawako tena
katika bendi hiyo, hivyo watakuwa huru kuungana na mwimbaji huyo mkongwe
na kushusha burudani nzito.


0 comments:
Post a Comment