Na Ashura Mohamed – Arusha
Msanii
wa muziki wa Kizazi kipya Diamond Platnum anatarajia kupagawisha
mashabiki wake wa jiji la Arusha siku ya Jumamosi ya tarehe 30
katika viwanja vya Hoteli ya Mount Meru.
Akizungumza
na waandishi wa habari muandaji wa shoo hiyo Faustine Mwandago ambaye
ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwandago Investment alisema kuwa maandalizi
yote ya awali ya shoo hiyo iliyopewa jina la Usiku wa Wasafi na
itakata kiu ya mashabiki wa Diamond waliopo jijini hapa.
Alisema
kuwa msanii huyo ambaye ni maarufu ambaye anasifika kwa kutoa burudani
ya nguvu pindi anapokuwa jukwaani yupo tayari kutoa burudani ya aina
yake na anatarajiwa kuwasili jijini hapa siku ya siku ya Ijumaa.
Aidha
mwandago alisema kuwa shoo hiyo ni ya aina yake kwa kuwa Diamond
hajawahi kuja kwa ajili ya kufanya burudani kwa muda mrefu hivyo basi
shoo hiyo ni kwa ajili ya kutoa burudani kwa mashabiki wake.
“Tumezoea
kumuona Diamond kwenye shoo za Mamiss kama Miss Arusha na nyinginezo
lakini kwa sasa hivi anakuja kwa ajili ya kutoa burudani tu kwa
mashabiki wake hivyo naamini kuwa shoo hiyo itakata kiu kwa
watakaohudhuria.”alisema mwandago
Akifafanua kuhusu shoo hiyo Mwandago alisema kuwa vazi litakalovaliwa kwa siku hiyo ni jeupe kwa kuwa ni Usiku wa Wasafi.
“Unapozungumzia
vazi jeupe maana yake ni lazima uwe msafi kwa kuwa halipendi bugudha
hivyo tumeona dress code iwe nyeupe ili tuwakilishe vyema jina la Shoo
la Usiku wa Wasafi”alisema Mwandago
Mbali
na burudani kutoka kwa msanii huyo wasanii wanaochipukia kama
Marry,Kandisi,Roggerz na madansasa wa boda boda waliopo chini ya
Mwandago Investment watapamba shoo hiyo.


0 comments:
Post a Comment