![]() |
ohn William `Del Piero`, kocha Njombe Mji fc |
J
KUFUATIA
soka la Tanzania kuendelea kukumbwa na vurugu za mashabiki hasa pale
timu zao zinapofanya vibaya, wadau wa soka waendelea kukiponda kizazi
cha wapenzi wa soka wa miaka ya leo kwa kukosa uvumilivu na kushindwa
kuelewa zana halisi ya michezo.
Kocha
wa timu ya soka ya Njombe mji inayoshiriki ligi ya mkoa wa Njombe na
mjumbe wa kamati ya ufundi ya klabu ya Simba Sc na mdau wa siku nyingi
wa soka la Tanzania, John W iliam maarufu kwa jina la `Del Piero`
amelaani vurugu zinazofanywa na mashabiki wa soka hapa nchini.
Piero
amesema hayo baada ya kushuhudiwa vurugu kubwa zilizofanywa na
mashabiki wa klabu ya Njombe Stand FC wakati wa mchezo wa ligi ya mkoa
wa Njombe mara baada ya kufungwa mabao 3-0 mpaka dakika ya 60, hivyo
kundi kundi kubwa la mashabiki lilivamia uwanja.
“Jana
(juzi) tulikuwa na mchezo dhidi ya Njombe Stand fc, ni mechi ya watani
wa jadi, mpaka dakika 45 timu hizi zilikuwa suluhu, kipindi cha pili
timu yangu ilipata mabao matatu ya haraka na ndipo mashabiki walipoanza
vurugu kwa kutoridhishwa na matokeo. Tabia hii si ya kimichezo kabisa”.
Alisema Piero.
Piero
alisema vurugu hizo sio tu kwa ngazi ya chini, bali hata ligi kuu
kumekuwepo na mwendelezo wa matukio kama hayo ya utovu wa nidhamu katika
soka.
Ametolea
mfano pale mashabiki wa Yanga walipofanya vurugu na kupasua vioo vya
gari la Coastal Union baada ya sare ya 1-1 uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam, pia mashabiki wa Simba jana walifanya vurugu na kung`oa baadhi
ya viti vya uwanja wa Taifa kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya Kagera Sugar
kwenye uwanja huo huo wa Taifa.

Mashabiki
wanaodhaniwa kuwa wa Simba sc jana walinyofoa viti vya kutosha uwanja
wa Taifa baada ya sare ya 1-1 na Kagera Sugar. (Picha na Bin Zubeiry)
“Mashabiki
wa timu kubwa za Simba na Yanga wanaona kuwa wao ndio wenye haki ya
kushinda, kumbe siku hizi mpira hauko hivyo, unaweza kuwa na uwezo
mkubwa na wachezaji wakubwa, lakini ukafungwa. kila timu inaingia
uwanjani kushindana, hivyo mashabiki wawe na moyo wa kukubali matokeo”.
Alisema Piero.
Pia
Piero amegusia vurugu zilizotokea mkoani Mbeya ambapo Yanga walifanyiwa
mchezo mchafu na mashabiki wa Mbeya City kwa kupasuliwa kioo cha mbele
upande wa dereva wa basi lao , lakini pia wiki hii wamewafanyia
Tanzania Prisons vurugu hizo nje ya uwanja wakati timu hiyo inarudi
kambini.
“Tatizo
la mashabiki wa soka wa Tanzania wanakwenda uwanjani na matokeo yao na
inapokuwa kinyume wanafanya vurugu nje ya uwanja, watu hawa wapewe
semina na vyombo vya usalama vitumie mamlaka yao kuwadhibiti watu hawa
wanaochafua taswira ya soka la Tanzania”.
“Binafsi
namuomba Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi na kamati zake kulichukulia
uzito suala la vurugu kwani ipo siku kutatokea maafa makubwa zaidi kama
ilivyowahi kutoka kwa nchi za wenzetu mfano Misri, Senegal na
kwingineko”. Alisema Piero.
0 comments:
Post a Comment