Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans wanaonolewa
na kocha Mholanzi, Ernie Brands akisaidiwa na Mtanzania Fredy Ferlicx
Minziro Katalaiya Majeshi Baba Isaya wanaingia kibaruani leo hii uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam kukabiliana na wapiga kwata wa JKT Ruvu
kutoka mkaoani Pwani.
Afisa habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto ameuambia mtandao wa FULLSHANGWE
kuwa maandalizi kwa ajili ya mechi hiyo yamekamilika na wachezaji wapo
katika hali nzuri ya kutafuta ushindi wa tatu mfululizo..
“Kama
iilivyo kawaida, Yanga ni timu inayocheza soka safi, tumejiandaa vizuri
kuchukua pointi tatu muhimu leo hii na kupanda kileleni mwa ligi kuu
soka Tanzania bara kwa mara ya kwanza tangu msimu wa mwaka huu kuanza”.
Alisema Kizuguto.
Kizuguto alisema kikosi cha Yanga kina wachezaji wengi wenye uwezo na leo hii ni chaguo la kocha Brandts kuamua nani anaanza.
“Nawaombe
mashabiki wa Yanga, timu ya wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia
soka safi la kikosi chao kilichoimarika kila idara, tupo kamili gado”.
Alisema Kizuguto.
Mara
baada ya ushindi wa pili mfululizo wa mabao 3-0 dhidi ya Rhino Rangers
na Mgambo Shooting kikosi cha mholanzi Ernie Brandts kimeendelea
kuimarika na safu ya ulinzi ikicheza michezo miwili pasipo kuruhusu
nyavu zake kutikiswa.
Mpaka
sasa Young Africans inashika nafasi ya tatu ikiwa na ponti 22 pointi 1
nyuma ya timu zinaongoza mbili za Azam FC na Mbeya City zote zikiwa na
pointi 23 zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Young
Africans inahitaji pointi tatu muhimu katika mchezo huo wa leo dhidi ya
JKT Ruvu ili iweze kujikita kileleni na kukalia kiti cha uongozi wa
Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 25 ambazo zitaweza kufikiwa na timu mbili
tu za Azam FC na Mbeya City ambazo zitachezwa mwishoni mwa wiki.
Timu
iliingia kambini juzi jioni katika hostel zilizopo makao makuu ya klabu
mitaa ya Twiga/Jangwani kujiandaa na mchezo huo ambao ni muhimu kwa
vijana wa Jagwani kuhakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi na kupata
pointi tatu muhimu.
Katika
mchezo wa leo Young Africans itakosa huduma ya wachezaji wake David
Luhende na Nizar Khalfani ambao ni majeruhi huku kiungo Haruna Niyonzima
akiukosa mchezo huo kutokana na kuwa nchini Rwanda alipokwenda
kushugulikia matatizo ya kifamilia.
Nao
JKT Ruvu kupitia kwa kocha msaidizi, Geryson Haule wametamba kupambana
mwanzo mwisho kuhakikisha wanaibuka na ushindi mbele ya Yanga.
“Yanga
ni bora, hilo halina ubishi. Lakini leo hii tutakwepa kuwa ngazi ya
kuchukulia pointi tatu na kuwapa nafasi ya kuongoza ligi”. Alisema
Haule.
Kocha
huyo alisema kikosi chao awali kilikuwa kinasumbuliwa na majeruhi,
lakini sasa kimekuwa sawa baada ya mabeki wake wa kati kupona na kurejea
uwanjani.
0 comments:
Post a Comment