Na Princess Asia,
KLABU
ya Yanga SC imetangaza rasmi kumuajiri Mkenya, Patrick Naggi, na watu
wengine wawili, ingawa imesema Lawrence Mwalusako ataendelea kukaimu
nafasi ya Katibu Mkuu wa klabu.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga amesema kwamba uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji jana mjini Dar es Salaam.
Sanga amewaambia Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kwamba Naggi ameajiriwa katika uongozi wa Yanga pamoja na Beno Salvatory Njovu (Mshauri wa Mambo ya Utawala na Fedha) na George Simba Magani atakayefanya shughuli za masoko.
Sanga amesema kwamba waajiriwa wote hao wapya, nafasi zao rasmi zitatangazwa baada ya miezi miwili, wakati Mwalusako anaendelea kukaimu Ukatibu, wakati mchakato wa ajira rasmi ya nafasi yake unaendelea.
Naggi
|

CHANZO:BIN ZUBEIRY
0 comments:
Post a Comment