NA ELEUTERI MANGI –MAELEZO
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amepokea
hati za utambulisho za Balozi mpya wa Italia katika Tanzania Dkt. Luigi
Scotto.
Mapokezi hayo yalifanyika katika halfa fupi iliyofanyika Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Rais
Kikwete amemtaka Balozi huyo mpya kuisaidia kuyashawishi makampuni
zaidi ya Italia kuja kuwekeza na kuboresha mahusiano ya kiuchumi wa
baina ya nchi hizo mbili.
“Tumekuwa
na makampuni makubwa ya Italia yaliyopata kuwekeza katika uchumi wa
Tanzania ikiwa ni pamoja na Agip na Incar lakini bado tunahitaji
uwekezaji zaidi ili tuweze kuimarisha zaidi uchumi wetu,” Rais Kikwete
alimwambia Dkt. Scotto.
Aidha,
Rais Kikwete ameishukuru Italia kwa misaada ambayo nchi hiyo imekuwa
inatoa kuchangia maendeleo ya Tanzania ikiwamo kugharimia ujenzi wa
Barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo.
Naye Balozi huyo mpya kwa upande wake amesema kuwa amefurahi kuteuliwa kuwa Balozi katika Tanzania.
“Ndoto
yangu kubwa tokea nikiwa mtoto ilikuwa ni kufanya kazi katika nchi
iliyomtoa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere” alisema Balozi Scotto.
Balozi
huyo alipowasili katika viwaja vya Ikulu alipokewa na wenyeji wake na
nyimbo za mataifa hayo ziliimbwa zikiongozwa na bendi maalumu
iliyoandaliwa kwa ajili ya mapokezi ya balozi.
Balozi
Dkt. Scotto anachukua nafasi ya mtangulizi wake nchini Perluigi Velardi
aliyemaliza muda wake wa kulitumikia taifa lake nchini.
0 comments:
Post a Comment