Mkuu
 wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akishiriki kwa vitendo 
kufyatua matofali na vijana wa CCM walioweka kambi katika Halmashauri ya
 Wilaya ya Sumbawanga katika Mji mdogo wa laela tarehe 22 Septemba 2013. Lengo
 kuu la kambi hiyo ni kuwajenga vijana katika itikadi na sera za Chama 
cha Mapinduzi, Ukakamau na Uzalendo kwa chama na nchi yao kwa ujumla. 
Katika kambi hiyo wanajishughulisha pia na kazi za kijamii kama 
kufyatua matofali zaidi ya 6,000 yatakayosaidia katika kujenga kituo cha
 afya Laela. Katika kuwapa nguvu kuendeleza kambi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa mchango wa laki mbili taslim.
Mkuu
 wa Mkoa wa Rukwa ambae pia ni Mbunge viti maalum CCM Mkoa wa Ruvuma 
akiwahamsisha vijana hao kukipenda chama chao kwa kuweka uzalendo mbele 
katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Chama hicho katika mji mdogo 
wa Laela tarehe 22 Septemba 2013. Kutoka
 kushoto ni Matin Matete Mjumbe wa baraza kuu CCM taifa, C. Bakuli 
Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Rukwa, Injinia Manyanya RC Rukwa, Godwin 
Mzurikwao Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Rukwa, Ali Mgaya Katibu wa Vijana 
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini na Persin Kalikule 
Mhamasishaji UVCCM Mkoa wa Rukwa.
Sehemu
 ya vijana hao waliotoka katika maeneo tofauti ya Halmashauri ya Wilaya 
ya Sumbawanga wakionekana kuhamasika vya kutosha katika kambi hiyo 
iliyopo katika mji mdgo wa Laela. 
Mwenyekiti
 wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Rukwa (UVCCM) Godwin Mzurikwao  
akielezea mipango mbalimbali ya umoja huo ikiwemo uhamasishaji na 
upandaji miti ya mbao kwa ajili ya kuwainua vijana kiuchumi Mkoani 
Rukwa. Katikati akisikiliza kwa umakini ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia
 Stella Manyanya. 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimkabidhi ndugu Ali Mgaya Katibu wa Vijana Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Vijijini miti na viriba
 vya kupandia miti ya mbao ambayo ni sehemu ya mpango wa UVCCM Mkoa wa 
Rukwa kuwawezesha na kuwahamasisha vijana katika zoezi la upandaji miti 
wa kibiashara.
(Picha na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa….rukwareview.blogspot.com)






0 comments:
Post a Comment