![]()  | 
| Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga | 
SHIRIKISHO LA NGUMI TANZANIA
Taarifa kwa vyombo vya habari. 
Yah:- BFT kutotambua viongozi waliojivika uongozi wa kuongoza Chama cha
ngumi Mkoa wa Dar es alaam (DABA) 21 SEPT. 2013. 
Shirikisho
 la ngumi Tanzania (BFT) halitambui uongozi uliojiingiza  madarakani wa 
kuongoza  chama cha ngumi mkoa wa Dar es salaam ( DABA ) kiujanja ujanja
 bila kuzingatia Sheria na Kanuni za Baraza la Michezo Tanzania (BMT) , 
katiba ya Chama cha ngumi cha dunia  (AIBA), Shirikisho la ngumi 
Tanzania (BFT) na katiba ya Chama cha Ngumi mkoa wa Dar es salaam 
(DABA).
Uongozi
 huo ulijingiza madarakani tarehe 21/09/2013 katika ukumbi wa DDC 
Mlimani bila ya kuwa na kibali cha kutoka BFT wala Kibali kutoka Ofisi 
ya afisa michezo wa mkoa wa Dar es salaam, ambao wao kiutaratibu ndio 
walikuwa na mamlaka ya kutoa kibali cha Kufanyika kwa uchaguzi huo na 
kuusimamia  kwa mujibiu wa sheria zinazoongoza michezo hapa Tanzania.
Badala
 yake genge la watu wachache walijikusanya na kupeana fomu kinyume na 
taratibu kwa kujuana na hatimaye kupeana taarifa wakakutana na kujivika 
madaraka kwa nyadhifa mbalimbali bila kufata taratibu.
BFT
 haikubaliani na jambo hilo kwa kuwa kati ya  waratibu wa zoezi hilo 
waliojivika uongozi wa juu ni wale waliokuwa katika uongozi wa 
shirikisho la ngumi Tanzania BFT na kupelekea Tanzania kufungiwa 
uanachama na chama cha ngumi cha dunia (AIBA) kwa miaka miwili na zaidi 
kusababisha bondia aliyekuwa  tegemeo na Taifa Petro Mtagwa kufungwa 
jela miaka 15 nchini Mauritius pia kusababisha bondia Emillian Patrick 
kushindwa kushiriki Mashindano ya Olimpiki 2008 baada ya kuwa amefuzu 
kwa tuhuma za kula njama za kusafirisha madawa ya kulevya.
Kibaya
 zaidi wengi waliopewa madaraka hawakuja fomu za kuomba nafasi kama 
walivyopewa na  hawakuwepo katika uchaguzi huo, wala hawakufanya usaili 
kama taratibu zilivyo. 
Wanachama
 halali waliokuwa wanatakiwa kuwepo katika uchaguzi huo mfano viongozi 
wa chama cha ngumi Temeke hawakupewa taarifa za uchaguzi na wameleta 
malalamiko ofisi za BFT.
Uchaguzi
 huo umekiuka katiba kwa  kuhusisha mabondia na viongozi wa ngumi za 
kulipwa kitu ambacho ni tofauti na katiba zote za ngumi za ridhaa.
BFT
 itachukua hatua kali za kimaadili na kinidhamu kwa wote waliohusika na 
zoezi hilo na kusisitiza kwa wanachama wote kuzingatia sheria za 
uchaguzi wanapofanya uchaguzi wa vyama vyao na kuwataka wengine 
kutokujiingiza kwa magenge ambayo historia inaonyesha wamekuwa wasubufu 
wa mambo mbalimbali tokea uongozi wa Narcis Tarimo enzi za TABA kwa 
masilahi yao binafsi.
Zaidi
 tutashirikiana na Ofisi ya Afisa michezo wa Mkoa kuhakikisha uchaguzi 
unafanyika wa kupata viongozi  kwa kuzingatia taratibu.
Taarifa hizi zinaletwa kwenu na 
Makore Mashaga
Katibu Mkuu.


0 comments:
Post a Comment