Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo(WAMA) akisalimiana na viongozi wa wilaya ya
Kisarawe hivi karibuni wakati alipowasili katika Shule ya Sekondari
Msimbu iliyopo wilaya hiyo mkoani Pwani ili kuzungumza na wanafunzi wa
shule hiyo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario .

Mkuu
wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario akisisitiza jambo wakati Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete alipotembelea Shule ya Sekondari Msimbu na
kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambapo aliwaasa wapende shule na
kuepukana na mambo mabaya kama vile mafataki na uvutaji bangi ili waweze
kufikia malengo waliojiwekea,kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)
anayefuatia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba na kulia ni
Mwenyekiti wa CCM Kisarawe Bi.Tatu Kano.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo(WAMA) akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari
Msimbu iliyopo wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wakati alipowatembelea
hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya kisarawe Fatuma Kimario,na
kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba anayefuatiwa Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri Zipporah Simwanza.

Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo(WAMA) akizungumza hivi karibuni na wanafunzi wa
Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani juu
ya umuhimu wa elimu na athari za mimba za utotoni wakati alipowatembelea
wanafunzi hao.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Msimbu wakisoma shairi la kumkaribisha Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake
na Maendeleo(WAMA) hivi karibuni wakati alipoitembelea shule hiyo
iliyopo wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

(Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)
0 comments:
Post a Comment