Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KLABU ya Arsenal amemsajili nyota wa Reak Madrid, Mesut Ozil kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni42.5.
Nyota huyo raia wa Ujerumani amesaini mkataba wa miaka mitano na mshahara wa pauni laki mbili na elfu 40.
Kiungo huyo amepima vipimo vya afya leo nchini Ujerumani, na licha ya Saint-Germain kutaja ofa nzuri zaidi mapema leo, nyota huyo ameamua kujiunga na washika bunduki wa London.
Kocha wa Arsenal , Arsene Wenger alimtafuta nyota huyo miaka sita iliyopita, lakini sasa Ozil ameshawishiwa na Mjerumani mwenzake Per Mertesacker na kocha Wenger mwenyewe.



0 comments:
Post a Comment