Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akitia saini katika mpira wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano ya mpira wa Miguu ya Amani na Umoja Super Cup jijini Dar es Salaam jana. Mashindano hayo yanaratibiwa na Kikundi cha vijana cha Mambo Safi kilichopo Kimara Baruti chini ya udhamini wa waziri Mukangara ambapo jumla ya timu 32 kutoka jimbo la Ubungo zinashiriki mashindano hayo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu zinazoshiriki mashindano ya Amani na Umoja Super Cup wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akipokea risala kutoka kwa Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Amani na Umoja Super Cup Bwana Laurent Mtoi alipokuwa mgeni rasmi wa hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akipiga mpira ikiwa ni ishara ya kufungua rasmi mashindano ya Amani na Umoja Super Cup wakati alipokuwa mgeni rasmio katika uzinduzi wa mashindano hayo jana jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Florida FC ambao ni washiriki wa mashindano hayo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi ya ufunguzi mashindano ya Amani na Umoja Super Cup yaliyozinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara.
Wachezaji wa timu ya Kimara United ambao ni washiriki wa mashindano hayo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi ya ufunguzi mashindano ya Amani na Umoja Super Cup yaliyozinduliwa rasmi jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara akisalimiana na mashabiki waliofurika uwanja wa Kimara Baruti kushuhudia uzinduzi wa mashindano ya mpira wa Miguu ya Amani na Umoja Super Cup jijini Dar es Salaam jana. Mashindano hayo yanaratibiwa na Kikundi cha vijana cha Mambo Safi kilichopo Kimara Baruti chini ya udhamini wa waziri Mukangara ambapo jumla ya timu 32 kutoka jimbo la Ubungo zinashiriki mashindano hayo.
Picha Zote na Frank Shija – Maelezo
Na Frank Shija – Maelezo
Vijana waaswa kutokubali kutumiwa na watu kwa maslahi yao binafsi kwa visingizio vya siasa au dini, badala yake wajielekeze katika shughuli zitakazowaletea manufaa wao wenyewe ikiwemo kushiriki katika michezo na shughuli za uzalishaji mali.
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara alipokuwa akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa mashindano ya mpira wa miguu yanayojulikana kwa jina la Amani na Umoja Super Cup mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake Waziri Mukangara amesema kuwa inasikitisha kuona vijana wengi wanaharibikiwa na kuingia katika matatizo kwa kukubali kutumika na watu wachache kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kubebeshwa madawa ya kulevya na kushirikishwa katika maandamano pasipo kujua msingi wake.
“Ndugu zangu wana Ubungo hasa Vijana msikubali kuingizwa katika vitendo vya matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya na matendo mengine hasi kwa maendeleo yenu. Nawaomba tuwe waangalifu sana kwani vitendo hivyo vinawaharibia sifa yenu kama vijan na kama watanzania na hivyo kuwakosesha fursa za ajira zenye staha na heshima yenu katika jamii yetu na kimataifa.” Alisema Waziri Mukangara.
Waziri Mukangara ameongeza kuwa Serikali imejipanga kukabiliana na matendo hayo maovu katika jamii yetu na kusema kuwa ili kufanikisha mapambano hayo mchango wa vijana unategemewa kwa kiasi kikubwa hivyo amewaomba vijana kote nchinin kuunga mkono juhudi za Serikali yao katika kupambana na uhalifu wenye nia ya kubomoa amani ya taifa letu..
Mashindano ya Amani na Umoja Super Cup 2013 ni mashindano yaliyobuniwa na vijana wazalendo kupitia kikundi chao cha Mambo Safi chenye maskani yake Kimara Baruti jijini Dar es Salaa, mashindano yanajumuisha jumla ya timu 32 kutoka katika jimbo la Ubungo na baadhi ya timu kutoka Kinondoni wakiwa na lengo la kujenga na kuibua hari ya udugu, amani, umoja na mshikamano miongoni mwa jamii yetu.
0 comments:
Post a Comment