Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney hatimaye amekubali kubaki na kukubali ukweli kuwa hawezi kuruhusiwa kuihama klabu yake na kujiunga na Chelsea.
Japokuwa ameonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Jose Mourinho, Rooney ameamua kutulia ili aimarike zaidi baada ya kukosa mechi zote za maandalizi ya msimu mpya kutokana na kukumbwa na majeruhi.
Nyota huyo kwa mara ya kwanza alicheza jana chini ya kocha David Moyes katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu dhidi ya Swensea City ambapo United walishinda kwa mabao 4-1, huku akitoa pasi mbili zilizozaa mabao, lakini hakujiunga na wenzake kushangilia mabao hayo.




0 comments:
Post a Comment