


Kibada wakibada, Katavi
POLISI mkoani Katavi imeubaini mtandao wa matapeli uliojitanua katika mkoani humo pia katika mikoa ya Rukwa na Mwanza kwa kuwatia nguvuni vinara wake akiwemo mwanamke mmoja wakituhumiwa kutapeli watu kwa kujifanya wanatoa huduma za uganga wa jadi pasipo kuwa na kibali .
Kamanda wa Polisi mkoani hapa , Dhahiri Kidavashari aliwataja vinara wa matandao huo wa kitapeli kuwa ni pamoja na Issa Hassan(42) ,Hussein Hassan maarufu Rwango (38) wakiwa wakazi wa jijiji la Mwanza,na Magreth Bakari (45) mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa mjini Mpanda mkoani Katavi Charles Mwelela (38.)akiwa ni mkazi wa sumbawanga mkoani Rukwa.
Alibainisha hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake huku akiwaonesha watuhumiwa hao wanne pia tunguli zao wanazodaiwa kuzitumia kutapeli wananchi mbalimbali nchini ambapo Agosti 26 mwaka huu , saa tano usiku watuhumiwa hao walikamatwa katika Mtaa wa Mji mwema mjini hapa katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Vatikani .
Miongoni mwa tunguli hizo alizozioensha kwa waandishi wa habari na baadhi ya maofisa wa polisi ni pamoja na ndege aliyekaushwa ambaye hutumika kwa kuwafanya wanaume watii kilas kitu wanachoamriwa na wake zao ikiwemo kupika hadi kufua nguo za wake zao .
Pia alionesha uga mweupe ambao watuhumiwa hao walikuwa wakitumia kuwalevya watu kwa kuwawekea kwenye vileo na kuwaibia fedha zao zote kisha hutokomea kusikojulikana pia wamekujwa wanawatapeli watu kwa kuwadanganya kuwa wana pasi ya Mjerumani ambayo ni feki ambao inauzwa kwa zaidi ya milioni 20 kwa madai kuwa ina uwezo wa ‘kuzalisha “mabilioni ya fedha . .
Kwa mujibu wa Kamanda huyo watuhumiwa hao wanadai kuhusishwa na matukio ya kitapeli ambapo baadhi ya wafanyabiashara kadhaa wametapeliwa mamilioni ya fedha baada ya kuwekewa unga mweupe wenye uwezo wa kumlaza mtu kwa saa kadhaa kabla hajazinduka .
“Uchunguzi wa awali wa kipoli umebai kuwa watuhumiwa hawa hutapeli wagtu kwa mtindo wa kuwapa madawa ya kulevya na muda mwingine huwa wanawatapeli watu kuwa wana wana pasi ya Mjerumani ambayo ni feki na kuwataka watoe fedha zao pasipokujua kuwa wanatapeliwa’ alisisitiza Kamanda Kidavashari .
0 comments:
Post a Comment