Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amewaonya wapinzani wake katika kinyang`anyiro cha kusaka taji la ligi kuu soka nchini England na ushindi wa jana wa mabao 2-0 dhidi ya wageni Hull City unawatahadharisha kuwa amerejea kupambana.
Mourinho jana alituma ujumbe kwa wapinzani wake wakubwa, Manchester United kwa ushindi huo, na amewaonya kuwa bado jaribio lake la kutaka kumsajili mshambuliaji wao Wayne Mark Rooney halijaisha, dhamira iko pale pale.
Bosi huyo wa Stamford Bridge amethibitisha kuwa atamfukuzia mshambuliaji huyo hadi mwisho wa dirisha la usajili majira haya ya kiangazi septemba 2 mwaka huu, na mtandao wa michezo waSportsmail unafahamu kuwa kama atashindwa kufanikiwa basi ataendelea kumshawishi wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi januari mwakani.

Mourinho amepunguza kumtaja Rooney lakini alisema: “Mnajua wachezaji gani tunawahitaji, tutakabiliana na suala hili lakini mara zote tutafuata taratibu zote”.
Klabu ya Chelsea inajiandaa kutuma ofa nyingine wiki hii inayosemekana kuwa pauni milioni 40 kumnasa nyota huyo wa Old Trafford.
Chelsea wanamfikiria Robert Lewandowski kuwa mbadala kama watamkosa Rooney, lakini nyota huyo amekubali kubakia Borussia Dortmund kwa mwaka mmoja kabla ya kujiunga na Bayern Munich mwaka ujao.
Wakati huo huo, Chelsea watakuwa na mazungumzo na wawakilishi wa Samuel Eto’o jumanne ya kesho ili kuona namna ya kumsajili

Hajatulia: Wayne Rooney aliitazama mechi ya ufunguzi wa ligi kuu soka nchini England dhidi ya Swansea kwa kipindi chote cha kwanza akiwa benchi


0 comments:
Post a Comment