Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsamail.com
KLABU ya zamani ya kocha , David Moyed, Everton imeripotiwa kuikataa vikali ofa ya pauni milioni 28million kutoka kwa mabingwa wa ligi kuu wa England, Manchester United kwa ajili ya kuwasajili beki Leighton Baines na kiungo matata Marouane Fellaini.
Mashetani wekundu wenye makazi yao Lod Trafford, walituma ofa ya pauni milioni 16 kwa ajili ya Fellaini – wiki mbili baada ya kumalizika kwa muda wa kutengua kipengele chake cha kumuuza kwa ada ya pauni milioni 23.5, na pia wakaongeza millioni £12 kwa ajili ya Baines, taarifa kwa mujibu wa Liverpool Echo.
Lakini Everton kwa haraka waliikataa ofa hiyo kutoka kwa kocha wao wa zamani David Moyes, siku mbili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England.
Inaaminika Everton watakuwa tayari kuwauza wachezaji hao angalau kwa bei ya kuanzia £38m na sasa inasubiriwa kama United watakuwa tayari kuongeza paundi millioni 10 ili kufanikisha dili hilo kabla ya siku 14 za dirisha la usajili hazijaisha.

Kiungo mtaalamu Marouane Fellaini


Leighton Baines
Nyota wawili: Kocha wa Manchester United David Moyes (pichani chini) anajaribu kuwasajili nyota wake wa zamani katika klabu ya Everton, Marouane Fellaini Leighton Baines kwa dau la pauni milioni 28m – lakini wakali hao wa Merseyside wamekataa ofa hiyo
Baada ya kushindwa kumsajili Cesc Fabregas, Thiago Alcantara na wachezaji wengine waliokuwa wanawahitaji majira haya ya kiangazi, sasa United wamegeukia kwa wachezaji wa Everton ili kuimarisha kikosi chao
Wamerudi kazini: Wote Baines (kushoto) na Fellaini walicheza katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu England dhidi ya Norwich City na kuambulia sare ya 2-2 katika dimba la Carrow Road jumamosi iliyopita.
Msimamo mkali: Kocha wa Everton, Roberto Martinez, anaonekana kutokuwa na presha ya kuwauza nyota wake
0 comments:
Post a Comment