Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA wa Chelsea , Mreno, Jose Mourinho ameanza kwa kishindo Stamford Bridge tangu arejea kwa mara ya pili baaada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu mpya ya ligi kuu soka nchini England, Hull City.
Ikiwa imepita takribani miaka sita tangu aondoke darajani na kurejea majira haya ya kiangazi, leo hii Mourinho alianza kibarua katika dimba la nyumbani na kushangiliwa na mashabiki lukuki wanaomuunga mkono kwa asilimia mia moja.
Katika mchezo huo, kiungo mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard alikosa mkwaju wa penati dakika ya sita baada ya kipa wa Hull, Allan McGregor kuokoa na baada ya hapo kipa huyo aliokoa tena mpira wa kichwa uliozamishwa na Branislav Ivanovic , lakini teknolojia ya goli iligoma na kuwaambia Chelsea sio goli.
Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na Oscar katika dakika ya 13 akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Kevin de Bruyne, na bao la pili limefungwa na Frank Lampard dakika ya 25 na kufuta makosa ya kukosa penati.


Kikosi cha Chelsea leo: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Lampard, Ramires, De Bruyne (Schurrle 67), Oscar (van Ginkel 85), Hazard, Torres (Lukaku 75)
Subs not used: Essien, Mata, Ba, Schwarzer
Goals: Oscar 13, Lampard 25
Kikosi cha Hull City: McGregor, Elmohamady, Chester, Davies, Figueroa, Brady, Meyler (Huddlestone 59), Koren, Sagbo, Graham (Livermore 59), Aluko (Boyd 79)
wachezaji wa akiba: Rosenior, Bruce, McShane, Harper
Kadi: Meyler
Mashabiki: 41,374
mwamuzi: Jon Moss

Mechi nyingine iliwakutanisha
Crystal Palace
| 0-1 |
Tottenham
|
0 comments:
Post a Comment