Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Katika
pita pita zangu ndani ya jiji la Dar es salaam na viunga vyake nikiwa
katika majukumu ya kutafuta habari kwa ajili ya wadau wa mtandao huu,
ghafla nakutana na mchezaji kinda wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Dar
Young Africans, Omega Seme, hivyo nalazimika kupiga nae stori mbili
tatu kabla ya kuendelea na mambo yangu.
Yafuatayo
ni mazungumzo yangu na Omega Seme, lakini Ijumaa ya wiki hii
tutaendelea nayo kwani kuna mambo amesema anaweka sawa. Karibu sana!.
Mpenja: Omega mambo vipi?
Omega: Safi jembe langu!
Mpenja: vipi mbona unaongea kama umechoka?
Omega: Nimetoka matizi kaka, so! napumzika kidogo hapa.
Mpenja: Ulikuwa mazoezi ya Yanga?
Omega: Hapana, nilikuwa napiga mazoezi binafsi tu, si unajua soka ni mazoezi kaka?, najiweka sawia.
Mpenja: Kuna taarifa kuwa unataka kutimkia Prisons, kweli?
Omega: Haijathibitishwa mpaka sasa ndugu yangu, subiri nitakuambia.
Mpenja: Mpango upo?
Omega: Upo sana mtu wangu, tulia tuli, nitakujuza mambo yakienda vizuri.
Mpenja: kwanini unataka kuihama Yanga?
Omega:
daaah! Hata wewe mwenyewe uliona mchezo ulivyokuwa unaenda, sikuwa na
nafasi, mchezaji yeyote anataka kucheza. Natafuta sehemu ya kucheza
mpira ili kuendeleza kipaji changu.
Mpenja: Kwahiyo mazungumzo na Prisons bado?
Omega: Nitakupa jibu Ijumaa ya wiki hii, kila kitu kitakuwa sawa. Nitakutafuta mwenyewe ili nikupe ishu.
Mpenja: Vipi Mipango yako msimu ujao?
Omega: Nalala naota mpira, soka ni kazi yangu, nahitaji kucheza, nikienda timu nyingine itakuwa nafasi nzuri kwangu kucheza.
Mpenja: Vipi Changamoto ya timu kubwa?
Omega:
Ni ngumu sana kupata nafasi, kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa hali
ya juu, lakini ni kawaida tu, ila inategemeana na maamuzi ya kocha.
Mpenja: Nitakutafuta Ijumaa nijue mpango wako wa kwenda Prisons, au vipi Omega?
Omega: Haina noma kaka, hata mimi nitakutafuta nikueleze.
Mpenja: Poa. Kila la heri na mchana mwema.
Omega: Asante na wewe pia. Karibu sana.
Msomaji
wa mtandao huu, subiri Ijumaa ya wiki hii, nitakutana na Omega seme ili
kunipa ukweli wa dili lake la kutaka kuihama Yanga na kutimkia Prisons.
Itaendelea Ijumaa…….
0 comments:
Post a Comment