Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Rais wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell, amethibitisha kuwa Tito Vilanova amebwaga manyanga kuifundisha klabu hiyo kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili kwa sasa.
Vilanova mwenye umri wa miaka 44, aliyerithi mikoba ya Pep Guardiola msimu uliopita amelazimika kujiuzulu kufuatia kuendelea kwa tatizo lake la saratani na mpaka sasa anajiandaa kwenda kupata matibabu nchini Marekani baada ya tatizo lake kujirudia tena.
Barcelona kupitia mtandao wao wa kiofisi wamesema: ’Tito Vilanova hataendelea kuwepo katika benchi la Barca”.
Rais Sandro Rosell ametangaza ijumaa ya leo kwamba kocha huyo wa wazee wa Katalunya hataweza kufundisha msimu ujao
Katika mkutano mfupi ambao viongozi wa bodi ya klabu ya Barcelona walikutana, Rosell alisema: “Habari nilizonazo ni zile ambazo hamtapenda kupokea”.
“Kufuatia kutathimini ratiba ya matibabu ya Tito, sasa mambo yamekuwa magumu zaidi, hataweza kuwa kocha mkuu”
Kwa heri ; Tito Vilanova akizungumza na wachezaji wake katika mazoezi ya jana
Huzuni kubwa: Sandro Rosell na Andoni Zubizarreta wamethibitisha kuondoka kwa kwa Vilanova
Rais wa Barca, Sandro Rosell na Mkurugenzi wa Michezo, Andoni Zubizarreta wamethibitisha kubwaga manyanga kwa Vilanova katika mkutano uliofanyika usiku huu.
Msaidizi wa Vilanova, kocha wa zamani wa Girona, Joan Francesc Ferrer ‘Rubi’, anatarajiwa kuteuliwa kocha wa muda wa dharula, wakati klabu ikitafuta kocha wa kudumu.
Kazi ngumu sana: Rosell atatafuta mrithi wa Vilanova
Daah! baba anasepa: Mchezaji muhimu wa Barca Lionel Messi anaweza kuathiriwa sana kuondoka kwa kocha wake
Afya mgogoro: Vilanova ameachia ngazi kuinoa Barca ili akatibu matatizo yake ya saratani
Haya sasa kazi kwako: Joan Francesc Ferrer anakabidhiwa matunguli ya Tito 
0 comments:
Post a Comment