Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
“Negredo, Sergio Aguero na Edin Dzeko ,Stevan Jovetic”. Washambuliaji hao wote wana viwango vya juu, sasa swali ni moja, nani kuwa chaguo namba moja kwa kocha mpya wa City, Manuel Pellegrini?.
Miamba ya soka nchini England na wenye jeuri ya pesa, klabu ya Manchester City imethibitisha kumsaini mshambuliaji hatari Stevan Jovetic kutoka Fiorentina kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 25.8 baada ya mwanandinga huyo wa kimataifa wa Montenegro kufuzu vipimo vya afya katika dimba maridhawa la Etihad.
Inaeleweka kuwa City watalipa kiasi cha Pauni Milioni 22.4 na ada itapanda kutokana na kukua kwa malipo ya posho ya nyota huyo mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu.
Pia Uhamisho wa nyota mwingine , Alvaro Negredo umethibitishwa, huku akikabidhiwa jezi namba tisa.




Karibu Manchester: Mshambuliaji raia wa Montenegrin, Jovetic akiwasili katika Hoteli ya Manchester jana usiku



Haina noma, barida tu!: Nyota huyo atapambana kutafuta namba pamoja na Negredo, Sergio Aguero na Edin Dzeko

Tayari ametulia zake: Jovetic amewasili katika klabu mpya ya City na sasa kilichobaki ni kushindana kupata nafasi kikosi cha kwanza
0 comments:
Post a Comment