Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa majogoo wa jiji, klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers amefunguka na kusisitiza kuwa mshambuliaji wake nyota raia wa Uruguay, Luis Suarez haondoki Anfield, huku akithibitisha kuwa anawasiliana na mkali huyo kila siku na hataki kumuuza katika majira haya ya joto ya usajili barani Ulaya.
“Nimezungumza na Luis tangia miezi michache iliyopita wakati kukiwa na taarifa nyingi kuhusu nyota huyo kuihama klabu hiyo kutokana na matatizo aliyokuwanayo” Rodgers amewaambia tlakSPORT.
“Lakini ukweli unabaki pale pale, tunamthamini mchezaji, alikuwa na msimu mzuri uliopita hapa klabuni na kuonesha ubora wake”
Rodgers aliongeza kuwa amekuwa na mawasiliano na Luis, kupitaa meseji na mazungumzo ya simu na mambo yanakwenda sawa; Ni mchezaji wa thamani, hakika ni mtu wa ajabu akiwa uwanjani.
Wakati kocha huyo wa wekundu wa Anfield akisema hayo, tayari washika bunduki wa London kaskazini, Asersal, walishatuma ofa ya pauni milioni 30 kutaka kumsajili Luis, lakini Liverpool walikataa ofa hiyo na kusisitiza kuwa hauzwi.
Suarez yupo mapumzikoni baada ya kutoka kuitumikia timu yake ya taifa ya Uruguay katika mashindano ya kombe la mabara nchini Brazil na Rodgers ana amini nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 atabakia kuwa mchezaji wa Liverpool na atarudi kwa ajili ya mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini Englnad julai 21 mwaka huu.



0 comments:
Post a Comment