Na Baraka Mpenja
Siku chache baada ya uongozi wa wekundu wa
Msimbazi Simba kumrejesha kundini kiungo wake mahiri mwenye uwezo mkubwa wa
kupaka rangi mpira, Ramadhan Suleiman Chombo “Redondo” amefunguka na kuweka
wazi kuwa nafasi hiyo ni muhimu kwake kwani bado anathimini mchezo wa soka kuwa
ni ajira yake rasmi inayomfanya ale, avae na kufanya mambo mengi yahusuyo maisha maisha yake.
Redondo aliyesimamishwa pamoja na wenzake , Washambuliaji,
Ferlix Sunzu na Abdallah Juma, mabeki Juma Nyoso, Paul Ngalema, na viungo Haruna
Moshi “Boban”, na Mwinyi Kazimoto
Mwitula, amerudishwa katika kikosi cha Abdallah Kibadeni, pamoja naye Kazimoto aliyerudishwa muda mrefu, wakati Sunzu alimaliza mkataba
wake na wengine wametemwa moja kwa moja.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI, Redondo amesema kusimamishwa kwake kulimuuma sana
kwani alikuwa mgonjwa baada ya kutoka Angola kucheza mechi ya ligi ya mabingwa
barani Afrika dhidi ya Libolo, mechi ambayo Simba walifungwa mabao 4-0.
“Unajua nilisimamishwaje ndugu yangu?,
tulipotoka Angola kucheza na Libolo na kurejea Dar es salaam, mimi ni Mwinyi
Kazimoto tulipata maleria, baada ya kupona na kwenda mazoezini, tukashangaa
kocha anasema hatutaki mazoezini na ndipo tuliposimamisha. Na wengine waliofuta
mbele yetu mfano Abdallah Juma wote walisimamishwa, niliumia sana, lakini
sikuwa na jinsi”. Alisema Redondo.
Redondo
aliongeza kuwa kurejea kwake Simba ni muhimu sana na atafanya vizuri na
kuwafurahisha mashabiki wa Simba ambao kwa sasa wana uchu mkubwa wa kuona timu
yao inafanya vizuri msimu ujao.
“Nitacheza kwa kujituma zaidi, nakumbuka siku
moja tuliwahi kuzungumza na wewe nikiwa Azam fc kuwa baada ya Kagame nitarudi
timu ya taifa, na ikatokea hivyo, nadhani unakumbuka, daima mimi najua mpira ni
kazi yangu, nitajituma zaidi kwa kuisaidia timu yangu”. Alisema Redondo.
Pia alisisitiza kuwa ifike wakati wachezaji
wanatakiwa kuthaminiwa sana kama nchini za wenzetu, hata zawadi wanazopewa
baada ya kufanya vizuri ni muhimu zikathaminiwa zaidi ili kuamsha ari ya mpira
wa Tanzania.
“Wakati nikiwa Azam, rafiki yangu Ngassa
alipewa kiatu dhahabu cha mfungaji bora, lakini ni kama mbao Fulani, kilichofanyika
ni kupuliziwa rangi ya dhahabu tu, nilimuuliza utaweka nyumbani kweli hii mwanangu?
Akaniambia hii kitu nitampa tu mwanangu achezee. Afrika kusini wenzetu
wameendelea, na sisi tuige mfano wao, tuthamini vipaji”. Alisisitiza Redondo.
Redondo alisema kuwa kuna wachezaji wengi wameacha
mpira bila sababu, na kitu kikubwa kinachowasababisha ni magumashi na fitina za
viongozi wa soka ambao mara zote hawathamini vipaji vya soka.
“Kwa mfano leo hii Shaban Kisiga wanamuita
mzee, lakini yule jamaa ni bonge la mchezaji, kushindwa kuthamini kipaji chake
ndio sababu ya kumuona kama hana maana. Sio yeye tu, wapo wengi zaidi ya yeye,
hata wewe unawajua ndugu yangu”. Alisema Redondo.
Wakati huo huo rafiki yake Redondo ambaye ni
shabiki wa kutupwa wa klabu ya Yanga ya Dar es salaam Bwana Yahya Uyagwa
alifurahishwa na kitendo cha rafiki yake kurudi Simba ili waandeleze utani wao.
“Mimi bwana nampenda sana huyu jamaa, mimi ni
shabiki wa Yanga, lakni Redondo ni mshikaji wangu wa kufu mtu, nimefurahi sana
kurejea Simba, nadhani atafanya vizuri kwani anajituma sana”. Alisema Uyagwa.
Uyagwa aliongeza kuwa mara nyingi Yanga
ikiwafunga Simba anamcheka sana Redondo, lakini yanaisha uwanjani na baada ya
hapo wanafikiria maisha mengine nje ya
mpira, ila amemsifu rafiki yake kwa kuwa mvumilivu na kujua kazi yake vizuri.
0 comments:
Post a Comment