Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mashetani wekundu, Manchester United, rasmi wamefungua njia kwa mshambuliaji wao Wayne Mark Rooney baada ya kusema hawana mpango wa kukaa chini na nyota huyo kuhusu kusaini mkataba mpya wa kuichezea klabu hiyo na wanachohitaji kwa sasa ni kumuangalia uwezo wake uwanjani kabla ya kukaa mezani kujadili hatima yake Old Trafford.
Mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward alithibitsha hilo jana wakati klabu yao ikishuka dimbani katika mchezo wa kwanza tangu waanze ziara yao nchini Thailand ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ambapo alisema kipaumbele kwa sasa nikuangalia dili la uhamisho kama litalipa na sio kuweka nguvu kubwa ya kukaa na Rooney kujadili hatima yake.
Roonye bado amebakiza miaka miwili katika mkataba wake ambao anakunja kitita cha pauni laki mbili na nusu kwa wiki.
Kwasasa mshambuliaji huyo amerudi nchini England baada ya kupata majeraha ya nyama za paja,huku akihusishwa na mpango wa kutimkia konako Chelsea au kwa matajiri wa Ufaransa , Paris St-Germain, lakini imeshaelezwa na United kuwa nyota huyo baba wa watoto wawili hatauzwa majira haya ya kiangazi.
Woodward alisema: ‘Hakuna majadiliano yoyote yaliyofanyika juu ya kuongezwa kwa mkataba. Sijakaa na mchezaji yeyote kujadili kuongeza mkataba wake na hakuna chochote kwenye kitabu changu cha kumbukumbu”
‘Tunaweza kuongopa kuvunjika kwa mkataba na Mchezaji? kiukweli hapana”.
Rooney hakuwepo katika kikosi cha jana cha David Moyes ambapo aliiongoza United katika mechi ya kwanza dhidi ya Singha All-Stars mjini Bangkok na kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Kauli hii ya kibosile huyo wa United imeongeza nguvu kwa kocha wa Chelsea, Jose Mourinho ambaye alisema yupo tayari kumwaga kitita cha pauni milioni 60 ili kumnasa Rooney, lakini naye Laurent Blanc wa PSG amekodoa macho yake kwa nyota huyo.









0 comments:
Post a Comment