Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Klabu ya Manchester United sasa imehamishia nguvu zake kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa FC Barcelona,Cesc Fabregas kwa dau la uhamisho la pauni milioni 26.
David Moyes kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na taarifa za kumtaka nahodha huyo wa zamani wa washika bunduki wa kaskazini mwa London, ikiwa ni harakati zake za kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England na ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Baada ya kumkosa mchezaji mwingine wa Barca, Thiago Alcantara mwenye umri wa miaka 21 aliyejiunga na mabingwa wa Bundesliga na UEFA, FC Bayern Munich, sasa mashetani hao wekundu wamehamishia mawindo kwa Fabregas raia wa Hispania.
Mkurugenzi mkuu wa United Ed Woodward siku za hivi karibuni alitamba kuwa kwa sasa klabu yake inaweza kumsajili mchezaji yeyote ambaye dau lake litakuwa kati ya pauni milioni 60 na 70, kikubwa kocha wao Moyes aseme anamtaka nani.
Woodward alisema: ‘kwa sasa tuna pesa ya kutosha mfukoni mwetu, lakini tunaenda kwa mipango kununua wachezaji na kama Moyes anataka kununua mchezaji yeyote atakayetaka, aseme tu”


Wametokelezea: Fabregas akiwasili na mpenzi wake Daniella Semaan katika harusi ya mchezaji mwenzake wa Barcelona Xavi jumamosi iliyopita
Endapo ofa hiyo ya pauni milioni 26 itakubaliwa na Barca, rekodi ya usajili wa Dimitar Berbatov wa pauni milioni 30.75 mwaka 2008 akitokea Tottenham itaendelea kudumu.
Fabregas alijiunga na Barcelona kutokea Arsenal mnamo mwaka 2011 kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 31 na Licha ya kuonesha kiwango kizuri, bado nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Barcelona imekuwa finyu sana.

0 comments:
Post a Comment