Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anaamini mapokezi makubwa aliyopata nyota wake, raia wa Uruguay, Luis Suarez wakati akirejea rasmi kazini leo hii yanaweza kumshawishi kubakia Anfield.
Suarez aliyekuwa akihusishwa kuhamia Arsenal, alipokelewa na mashabiki wapatao 95,446 wakati alipoingia dakika ya 72 na kutoao pasi ya bao katika ushindi wa 2-0 ilioupata klabu yake dhidi ya Melbourne Victoryuwanja wa MCG.
“Luis ameonekana kuwa na kasi na amedhihirisha kuwa atafanya vizuri zaidi mara msimu mpya utakaponaza”. Alisema Rodgers.
Rodgers aliongeza: ‘Sina kitu chochote cha kuongeza kuhusiana na (ofa ya Asernal). Kitu pekee ni uwepo wa mazungumzo kati ya Luis na mimi. Hakuna ubishi, siku hizi soko la wachezaji wakubwa ni dogo sana. Luis atakuwa akihusishwa tu na klabu kubwa”.
“Mashabiki walivyompokea wameonesha bado wanampenda licha ya kukosa mechi nyingi kutokana na sababu mbalimbali. Walisimama kwa ajili yake na kuonesha heshima kubwa kwake”.








0 comments:
Post a Comment