NYOTA
watano wa kimataifa wanaokipiga katika timu ya Azam fc ya Dar es
Salaam, maarufu kwa jina la wana lambalamba wanatarajiwa kuwasili nchini
leo kujiunga na wenzao kwa mazoezi ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Azam na timu nyingine za Ligi Kuu, zimeanza kujiandaa na ligi hiyo itakayoanza Agosti 24.
Katibu
mkuu wa klabu hiyo Alhaji Idrisa Nasoro amedokeza kuwa nyota hao
wanaorejea leo wakitokea kwenye mapumziko ni Kipre Tchetche na Kipre
Balou, raia wa Ivory Coast.
Aliwataja
wengine ni Humprey Mieno, Joackim Atudo kutoka Kenya na Brian Umony wa
Uganda, na kuongeza kuwa kuripoti kwa nyota hao ni faraja kubwa kwani
mazoezi yataanza kunoga.
Mbali
ya nyota wa kimataifa, pia wachezaji wengine wawili, David Mwantika na
Omari Mtaki waliokuwa na udhuru, pia wanatarajiwa kuripoti leo.
Alisema
mipango ya kwenda kujifua nchini Afrika Kusini kabla ya kuanza kwa ligi
hiyo haijabadilika. Wataondoka mwishoni mwa wiki hii.
Alisema
mipango ya safari hiyo inaendelea kupangwa na uongozi ikiwa ni pamoja
na sehemu ya kufikia na mechi za kirafiki watakazocheza wakiwa huko.
Msimu
uliopita Azam waliishia nafasi ya pili na hivyo kupata fursa ya
kuliwakilsiha taifa katika michuano ya kombe la shirikisho.
0 comments:
Post a Comment