Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Lejendari wa Manchester United, Ryan Giggs amekiri kuwa anashangazwa na kujishangaaa mwenyewe kwa kitendo chake cha kuendelea kuwa na uwezo mkubwa wa kucheza soka katika klabu yake na kufanikiwa kutwaa ubingwa mara 13.
Nyota huyo anayekaribia kufikisha umri wa miaka 40 anatarajia kuanza msimu wa 23 akiwa na United baada ya kuongezewa mkataba wa mwaka mmoja mnamo mwaka uliopita, hivyo kuendelea kuwa mtu muhimu katika kikosi cha mashetani hao wekundu wa England.
Baada ya leo United kuwasili Sydney nchini Australia kuendelea na ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini England, Giggs amesema anafurahia sana maisha yake katika klabu ya Manchester United.
Nafurahia maisha yangu kama nilivyofanya miaka 20 iliyopita. Ni rahisi sana kama mnavyoona. Kila mwaka kwangu ni zawadi kwangu. Chukulia mwaka uliopita: Nimebeba ubingwa wa ligi kuu, hakika kushinda baada ya kufanya kazi kubwa imekuwa ni heshima na thamani kubwa sana”.
“Kitu muhimu kwa Manchester United ni kutwaa mataji tena. Huu ni mwanzo wa safari ya mwaka mpya na natumaini kubeba ubingwa tena mwishoni mwa msimu ujao”. Alisema Giggs
‘The thing about Manchester United is you have to do it all over again. This is the start of the journey this season and I hope to be lifting a trophy again at the end of the season.
Giggs alitegemea kucheza katika mchezo wa jana dhidi ya Singha All-Stars ambao walipoteza kwa kufungwa bao 1-0,na ulikuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Moyes, lakini haikuwa hivyo.
Giggs alisema: “Maandalizi ya msimu mpya ni magumu kwa wachezaji. Mnahitaji kujifua kwa nguvu sana, hivyo ni ngumu kucheza na timu yenye ubora. Lakini tunaangalia mbele. Baada ya mchezo wa jana ambao tumepoteza, tutautumia kupata matokeo mazuri na timu kuimarika zaidi michezo ijao. Tunaangalia mbele zaidi.”
Anamwaga wino: Ryan Giggs akisaini kitabu cha kumbukumbu cha shabiki wa United mjini Sydney baada ya Manchester United kuwasili
Giggs akiangalia simu yake baada ya kupiga picha ya Sydney Opera House
Hapa ndipo tunaenda: Giggs akiwasili sehemu ambayo mkutano na waandishi wa habari uliandaliwa
Akichukua kumbukumbu: David Moyes alipiga picha bandari ya Sydney wakati akijiandaa kwenda katika mkutano na waandishi wa habari
Hii siiachi: Moyes akitumia simu yake ya mkononi kupiga picha baadhi ya maeneo mazuri nchini Australia
Sio uwanjani tu: Rio Ferdinand akirekodi video wakati United wakiondoka uwaja wa ndege
Wanasepa uwanjani: wachezaji wa United wanajiandaa upambana na A-League All Stars
Giggs akila pozi na shabiki wa United katika uwanja wa ndege wa Sydney
Muda wa kuzungumza: Moyes na Giggs wakiongea na waandishi wa habari nchini Australi
Ferdinand, Michael Carrick, Moyes na Giggs wakiwa katika picha ya pamoja 
0 comments:
Post a Comment