Na Baraka Mpenja
Wakata
miwa wa Kagera Sugar wenye makazi yao Kaitaba kanda ya ziwa mkoani
Kagera wamesema kocha wao mpya, Mganda Jackson Mayanja ambaye alikuwa
kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda ni bora zaidi ya Kibadeni
kwani yeye ndiye aliyesuka kikosi ambacho kocha huyo aliyetimkia kwa
wekundu wa msimbazi Simba alikiongoza msimu uliopita.
Afisa habari wa klabu hiyo, Hussein Mohamed amezungumza na MATUKIO DUNIANI
kwa njia ya simu kutoka Kaitaba na kubainisha kuwa klabu yao inatambua
sana mchango wa mwalimu Kibadeni, lakini aliwakuta wachezaji wameshaiva
baada ya kunolewa na kocha Mayanja, na sasa amerejea mwenye timu, hivyo
wana imani kubwa sana msimu ujao watafanya makubwa zaidi.
“Kwa
sasa tunaendelea na usajili wetu, kesho tunamalizana na mchezaji kutoka
Africa Lyon, Adam Kingwande ambaye tunaamini atatuongezea kasi zaidi
katika safu yetu ya ushambuliaji”. Alisema Mohamed.
Mohamed
alisema mazungumzo na Kingwande yamemalizika, huku akisema wanatambua
kuwa wana tatizo katika safu ya ushambuliaji, na suluhusho ni nyota huyo
mwenye makali ya kutosha.
“Timu
yetu haijabadilika sana, tumepoteza wachezaji wawili, kiungo Juma Nadi
aliyetimkia Ruvu Shooting na Andrew Ntalla aliyenaswa na Simba, hivyo
hatuna kazi kubwa sana ya kuziba nafasi”. Alisema Mohamed.
Afisa
habari huyo alisema timu hiyo itaanza mazoezi rasmi julai 10 mwaka huu
katika dimba la Kaitaba na kocha wao Mayanja anatarajiwa kuwasili kati
ya julai 8 tayari kwa kuanza program yake ya mazoezi.
Mohamed
alisisitiza kuwa msimu ujao wanajiandaa kuhakikisha wanashika nafasi
nzuri zaidi na kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa.
Msimu uliopita Kagera walimaliza ligi kuu wakiwa nafasi ya nne, huku Simba, Azam fc na Yanga wakiwa juu yao.
Mafaniko
hayo yalifikiwa chini ya kocha Abdallah Kibadeni “King Mputa” na sasa
kocha huyo mzawa amepata shavu kwa wekundu wa msimbazi ambaye ndiye
kocha mkuu.
0 comments:
Post a Comment