Na Baraka Mpenja
Timu
za netiboli za Jeshi la Polisi na Halmashauri ya jiji, mkoani Mbeya
zinatarajia kuanza mazoezi ya mapema ili kufanya vizuri katika michuano
ya ligi kuu daraja la kwanza ya mchezo wa mpira wa pete inayotarajiwa
kufanyika kwa mara ya pili mfululuzo jijini Mbeya kuanzia Agosti 24 hadi
septemba 7 mwaka huu.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka jijini Mbeya, mwenyekiti mwenye dhamana ya
kuongoza mchezo wa netiboli jijini humo, Mary Mng`ong`o ameipasha MATUKIO DUNIANI kuwa hakutakuwepo na ongezeko la timu za mkoa huo, lakini wanahakikisha timu wakilishi zinaanza maandalizi mapema.
“Tumelazimika
kuandaa michuano hii mikubwa ya kitaifa kwa mara nyingine, hatuna jinsi
kwani aliyekuwa mgeni rasmi mwaka jana, Naibu waziri wa Elimu na
Mafunzo ya ufundi, Mhe. Philp Mulugo alikitaka chama chetu kuandaa tena
kwa ufanasi zaidi. Tulikubali na sasa maandalizi yameshaanza”. Alisema
Mng`ong`o.
Kiongozi
huyo alisema Uongozi wa chama cha mkoa tayari umeshaziandikia klabu zao
barua ya kuanza maandalizi, huku wakiziomba kuandika barua na kutuma
CHANETA ili kuthibitisha ushiriki wao.
Mng`ong`o
alisema mwaka jana walikumbana na ukata mkubwa sana kuendesha
mashindano hayo, hivyo anawaomba wadau kujitokeza kwa wakati huu mgumu
kwao ili kuchangia na kufanikisha michuano hiyo kwa kiwango kukubwa
zaidi ya mwaka jana.
“Ndo
kwanza tunaanza kujipanga, wadau wana nafasi kubwa sana. Ni muhimu sana
kuchangia kwa moyo, kwani wakifanya hivyo basi kila kitu kitaenda
sawa”. Alisema Mng`ong`o.
Mwenyekiti huyo alisema tayari taarifa imeshatolewa kutoka CHANETA kuwa
Agosti 24 yataanza kutimua vumbi, na tayari uongozi wa chama hicho
chini ya mwenyekiti wake Anna Faith Kibira amesharidhia mkoa huo kuwa
mwenyeji wa michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment