Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha Arsene Wenger amepata pigo baada ya beki kisiki wa klabu hiyo, Laurent Koscielny kugongana na mlinda mlango Wojciech Szczesny na kuumia, hivyo atakaa nje ya uwanja katika mchezo wa kirafiki wa kesho mjini Nagoya.
Beki huyo alitoka katika mazoezi mwishoni na kuonekana mwenye maumivu ya kifundo cha mguu.
Timu ya matibabu wa Asernal walimchunguza tatizo lake kabla ya kuondolewa katika dimba la Mizuno Rugby kwa ajili ya matibabu zaidi.
Inafahamika kuwa nyota huyo alikuwa na maumivu tangu wawasili ijumaa nchini Japan.
Hata hivyo Lukasz Fabianski au Damien Martinez watachukua nafasi ya Szczesny katika mechi dhidi ya Nagoya Grampus.
Taarifa za kuumia kwa Koscielny zinamaanisha Wenger atamkosa moja ya mabeki wake wenye uzoefu, Per Mertesacker; katika ziara yake ya mashariki ya mbali, ingawa atamtumia zaidi kinda wake Ignasi Miquel
Wenger tayari hanaye Thomas Vermaelen, ambaye tupo nje ya uwanja kwa miezi mitatu.




Anatoa maelekezo: Arsene Wenger akizungumza na mashabiki wakati wa mazoezi




Furaha kubwa kuwepo hapa: Nyota wa England, Alex Oxlade-Chamberlain na Theo Walcott wakipozi katika picha wakati wa mazoezi



Majeruhi ya Koscielny yatamfanya kocha Wenger aongeze haraka kumsajili beki wa muda mrefu ambaye amuwania kutoka Swansea City, Ashley, Williams.
0 comments:
Post a Comment