Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Beki 
mkongwe wa mabingwa wa soka nchini England, Manchester United, Rio 
Ferdinand amesema kuwa endapo wachezaji Cesc Fabregas na Robert 
Lewandowski ambao wamekuwa gumzo kubwa katika heka heka za usajili 
barani ulaya, watakuwa wachezaji bora zaidi duniani kama watakubali 
kujiunga na klabu ya Manchester United.
Rio  
amesisitiza kuwa kama mchezaji yeyote anataka kuwa bora zaidi duniani, 
hana budi kupitia United, huku akimtolea mfano nyota wa sasa wa miamba 
ya soka nchini Hispania, Real Madrid, Mreno, Cristiano Ronaldo.
Fabregas
 mwenye umri wa miaka 26 na Lewandowski mwenye umri wa miaka 24 
wanatakiwa sana na kocha mpya wa Manchester United, David Moyes ili 
kuweza kutetea ubingwa wake msimu ujao.
Rio amesema “kama United wanakufuata mchezaji ili wakusajili, lazima ukubali kwani ni sehemu ya kuwa bora”.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa ameongeza kuwa wachezaji kama Ryan Giggs, Roy
 Keane, David Beckham, Andy Cole, wote wamekuwa wachezaji bora kupitia 
United, hivyo kama nyota hao watakubali kujiunga na mashetani wekundu 
watakuwa bora zaidi.
 
 
Ferdinand amesema kuwa wachezaji wapya wanaokuja United watapata makombe mengi zaidi chini ya kocha David Moyes
 
 
Muda si mrefu anatua kwa wekundu? Lewandowski na Fabregas wanaweza kujiunga na United majira ya joto ya usajili barani Ulaya 

 
 
Naye
 Cristiano Ronaldo aliyejipatia umaarufu mkubwa akiwa Manchester United 
anasemekana kurudi klabuni hapo kufuatia kukataa kusaini mkataba mpya 
Real Madrid.




0 comments:
Post a Comment