Chama
 Cha Mapinduzi (CCM) kimeitakia kila la kheri timu ya Taifa Stars ambayo
 inacheza  kutafuta tiketi ya kucheza kombe la dunia mwaka 2014. 
Taifa Stars katika mechi yake ya kesho itavaana na Timu ya taifa ya Morocco. 
Akizungumza
 kutoka Dar es salaam ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye 
alisema CCM inaitakia kila lakheri Taifa Stars na mafanikio katika 
mchezo wa kesho na kwamba CCM inatambua umuhimu wa taifa Stars kushinda 
mechi hiyo ya kesho.
Alisema anaamini dua za CCM na Watanzania wote zitaiwezesha Taifa Stars  kushinda mechi yake dhidi ya Morocco.
“Watanzania tunaomba muiombee Taifa Stars, tunaimani nayo, bila shaka itashinda kesho” alisisitiza Nape


0 comments:
Post a Comment