Monday, June 3, 2013

53

Na Baraka Mpenja
Wakati siku zinazidi kuyoyoma kwa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars kukabiliana na Simba wa milima ya Atlas mnamo juni 8 mwaka huu nchini Morroco, makocha mbalimbali wa soka wazidi kutoa tathmini yao kuhusiana na mchezo huo,  huku wengi wakiamini stars inaweza kupata matokeo mazuri ugenini.
Kocha mkuu wa maafande wa Ruvu Shooting wa mkoani Pwani na kocha wa zamani wa timu ya tifa ya wanawake “Twiga Stars”,  Charles Boniface Mkwasa “Masta” ameimabia MATUKIO DUNIANI kuwa matokeo ya jana usiku ambapo Stars ilitoka suluhu ya bila kufungana na Sudan hayana athari yoyote kwa kikosi cha Kim Paulsen ila yamempa nafasi ya kuona makosa ya timu yake.
Mkwasa amesema mara zote makocha wanatumia mechi za kirafiki kuangalia uwezo wa vikosi vyao, na kama timu imeshinda  mechi ya kirafiki inakuwa ngumu kuona makosa kirahisi, lakini inapopoteza mchezo inakuwa nzuri zaidi kugundua makosa.
Mkwasa alisema Sudan kwa sasa hawatishi sana, lakini mpira wao unafanana na wa Tanzania, mara nyingi Stars inakutana nao katika michauno ya kombe la CECAFA, hivyo matokeo ya jana ni ya kawaida.
“Malengo ya Stars sio kushinda mechi za kirafiki bali kuna mechi za mashindano ambazo mwalimu anazipa uzito mkubwa, kushindwa kuwafunga Sudan sio tatizo, kikubwa vijana wajengwe kuelekea mchezo wa juni 8 dhidi ya Morroco”. Alisema Mkwasa.
Kocha huyo aliongeza kuwa kuna wachezaji wawili wa safu ya ushambuliaji ambao walikosa mechi hiyo kutoka TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu , na watakapoongezeka kule Morroco timu itakuwa na nguvu zaidi kwani vijana hao wana uwezo mkubwa kwa sasa.
“Binafsi Morroco nawaheshimu sana, tuliwafunga nyumbani mabao 3-1, sio sababu ya kuwadharau, kinachotakiwa ni wachezaji wetu kupigania taifa na kuhakikisha wanashinda mechi hiyo ili kuendelea kujipatia matumaini makubwa ya kucheza fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil”. Alisema Mkwasa.
Mbali na Mkwasa, aliyekuwa kocha wa JKT Oljojoro na mchezaji wa zamani wa Taifa stars, Mbwana Makata amesema kuwa timu inapopoteza mchezo wa kirafiki wakati ikijiandaa na mechi ya mashindano ni vizuri zaidi kuliko kupata matokeo ya ushindi ambao yanaficha mabaya zaidi.
“Ukishinda unajiona unaweza na kubweteka, matokeo ya jana nimeyapenda, toka mwanzo nilikuwa naomba stars wasishinde ili mwalimu ajue cha kufanya, suluhu ya jana nadhani itawasaidia kupata nguvu mpya na kujiona wanahitaji kujituma”. Alisema Makata.
Makata alisisitiza kuwa kikosi cha stars kina morali kubwa, udhamini mnono, wachezaji vijana wenye nguvu na kasi kubwa, hivyo kuwabania Morroco na kuwatandika wakiwa kwao inawezekana kutegemeana na mazingira halisi ya huko.
“Nina imani na vijana wetu, sina shaka na kocha wetu, vijana wana mazingira mazuri sana, kila kitu kipo, morali ni kubwa tofauti na miaka ya nyuma, wamefanya vizuri mechi za kirafiki na kuzifunga timu kubwa wakiwemo Zambia na Cameroon, hii ni motisha tosha kabisa, kila la heri vijana wetu”. Alisema Makata.
Naye aliyekuwa kocha wa African Sports ya Tanga na sasa mjumbe wa kamati ya ufundi ya wekundu wa Msimbazi Simba, Mwalimu John Wiliam maarufu kwa jina la “Del Piero” amesema ushindi  katika mchezo wa Morroco uko pale pale kutokana na kocha wa Stars  kujua soka la wapinzani wake.
“Kim alienda Afrika kusini kuwatazama Morroco, wengi hawakujua maana ya ile ishu, hakika ilimpa uwezo mkubwa wa kuwajua wapinzania wake, madhaifu yao na makali yao, na ndio maana mechi ya kwanza aliwafunga kirahisi, sidhani kama wamebadilika sana, kikubwa ni vijana kuzingatia maelekezo ya mwalimu”. Alisema Piero.
Safari ya Brazil ipo na lazima Tanzania ifike huko, licha ya kupambana na timu kubwa wakiwemo Tembo wa Pwani ya magharibi ya Afrika,Ivory Coast, Gambia na waarabu wa Morocco.
Kila la heri taifa stars, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Taifa Stars.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video