Kaseja ambaye ni golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania kwa sasa yupo kwao mjini Kigoma alipoenda kupumzika baada ya kumaliza majukumu yake timu ya Taifa hivi karibuni, amezungumza na mwandishi wa mtandao huu Johnson Matinde akiwa kwao Kigoma kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kutemwa na Simba pamoja na mambo mengine.

Akizungumzia
kuhusu suala la kutoongezewa mkataba mpya na Simba, Juma Kaseja alisema
kwamba taarifa hizo yeye amezisikia kwenye vyombo vya habari kama watu
wengine walivyosikia na hajapata taarifa rasmi: "Jana nikiwa natokea
Tanga nilipokuwa nikapata taarifa za kuhusu masuala yangu na Simba.
Klabu kupitia viongozi wake imeshaongea kuhusu suala hili na mie itafika
siku nitaongelea kwa kina kuhusu jambo hili, ila kwa sasa ni kweli mimi
sio mchezaji wa Simba na nisingependa kuzungumzia kuhusu wao."
Akizungumzia kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kuachana na Simba, Kaseja alisema: "Mimi ni mchezaji mpira, hii ndio kazi yangu hivyo nitaendelea kucheza mpira. Sasa kama unavyoniona nipo hapa kwetu nafanya mazoezi ili niwe bora kwenye kazi yangu. Mengine kuhusu ni timu gani nitachezea msimu ujao ningependa tuyaache kwa sasa, utakapofikia muda muafaka wa kuzungumzia then nitaongelea jambo hilo."
Kaseja
akiwa mjini Kigoma amekuwa akijifua kwenye uwanja wa Shule ya msingi
Kaluta, shule ambayo Juma Kaseja alisoma na uwanja wa shule hiyo ndio
ambao alianzia career yake ya soka na ndio maana kila anapokwenda
mapumzikoni nyumbani kwao Kigoma hupenda kufanya mazoezi uwanjani hapo
na baadhi ya wachezaji chipukizi.
Akizungumzia kuhusu mustakabali wake wa soka baada ya kuachana na Simba, Kaseja alisema: "Mimi ni mchezaji mpira, hii ndio kazi yangu hivyo nitaendelea kucheza mpira. Sasa kama unavyoniona nipo hapa kwetu nafanya mazoezi ili niwe bora kwenye kazi yangu. Mengine kuhusu ni timu gani nitachezea msimu ujao ningependa tuyaache kwa sasa, utakapofikia muda muafaka wa kuzungumzia then nitaongelea jambo hilo."

HABARI KWA HISANI YA SHAFIH DAUDA
0 comments:
Post a Comment