
Na
Mtandao
Kwa mujibu wa orodha ya FIFA ya ubora wa soka duniani iliyotolewa
leo nchini Uswizi, zile timu zilizopo 3 Bora, Spain, Germnay na Argentina bado
zimeshikilia nafasi zao.
Tanzania inayoongozwa na taifa stars chini ya kocha mkuu Kim
Paulsen imepanda juu nafasi tatu na kujikita Nafasi ya 116.
Katika miezi miwili, Tanzania imepanda kwa kasi kutoka
nafasi ya 127 mwezi machi na kwenda nafasi ya 119 mwezi Aprili na sasa imekalia
nafasi ya 116 baada ya kushusha kipondo kwa Simba wasiofugika kutoka pwani ya magharibi
mwa Afrika, timu ya taifa ya Cameroon bao 1-0 uwanja wa taifa, na baadaye
kuwatungua simba wa milima ya Atlas, timu ya taifa ya Morroco mabao 3-1 katika
mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia.
Wakati Tanzania ikipanda nafasi tatu juu, Simba watatu yaani
timu ya taifa ya England imeporomoka nafasi 3 na sasa ipo nafasi ya 7 huku wazee
wa Samba na waandaaji wa michuano ya kombe la dunia mwakani, timu ya taifa ya Brazil
ikiporomoka nafasi 1 na sasa ipo ya 19.
Timu toka Barani Afrika ambayo iko juu sana ni Tembo wa
pwani ya magharibi ya Afrika, timu ya taifa ya Ivory Coast iliyopanda nafasi 1
na sasa ipo nafasi ya 12.
Orodha nyingine ya timu bora za taifa duniani itatolewa na
FIFA Mei 9 mwaka huu.
20
BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Argentina
4 Croatia
5 Portugal
6 Colombia
7 England
8 Italy
9 Netherlands
10 Ecuador
11 Russia
12 Côte d'Ivoire
13 Greece
14 Mexico
15 Switzerland
16 Belgium
17 Uruguay
18 France
19 Brazil
20 Denmark
0 comments:
Post a Comment