Na
mtandao
Mechi
za nusua fainali ya kombe la FA nchini Uingereza zinapigwa  zinachezwa leo Jumamosi na Jumapili Uwanjani
Wembley huku wachambuzi wa soka nchini humo wakiibatiza mechi ya kesho baina ya
Chelsea na Manchester city kuwa ndio mtanange wa `fainali`.
Leo
dimba la Wembley majira ya saa moja na robo usiku nusu fainali ya kwanza
itapigwa kwa kuwakutanisha wakali wa ligi daraja la chini Championship Millwall
dhidi ya timu ya ligi kuu Wigan Athletic.
Hapo
kesho kimbembe kitawaka tena kwa Chelsea na Man City kutunishiana msuli majira
ya saa 12 jioni.
Fainali
ya FA itashuhudiwa katika dimba la hilo la Taifa Wembley jumamosi ya mei 11
mwaka huu.
Millwall
v Wigan Athletic
Wigan wanatinga Wembley Jumamosi kucheza Nusu Fainali dhidi
ya Millwall, Klabu ya Daraja la chini Championship, lakini kibarua kikubwa kwa
Meneja Roberto MartÃnez ni kuinusuru Klabu kuporomoka Daraja kutoka BPL,
Barclays Premier League, ambako wako nafasi ya 18 wakiwa ni Timu ya 3 toka
mkiani.
Millwall, wakiwania kutinga Fainali yao ya pili katika Miaka
9, wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa nafasi ya 16 kwenye Ligi ya Championship.
VIKOSI
VINATARAJIWA KUTOKANA:
Wigan:
Robles,
Al Habsi, Boyce, Stam, Scharner, Caldwell, Golobart, Alcaraz, Figueroa,
Beausejour, McArthur, McCarthy, Gomez, Espinoza, Maloney, McManaman, Kone, Di
Santo, Henriquez.
Millwall:
Forde,
M Taylor, Dunne, Shittu, Lowry, Beevers, J Smith, A Smith, Osborne, St Ledger,
Malone, Wright, Abdou, Trotter, Feeney, C Taylor, Saville, N'Guessan, Marquis,
Batt, Keogh, Hulse.
Refa:
Michael
Oliver
 
Chelsea
v Man City
Manchester City na Chelsea wanaweza kupata mafanikio kwenye
FA CUP kwani kuna kina dalili Ubingwa wataukosa kwa vile Man United ndio
wanachanja mbuga na Nusu Fainali hii ni ‘PIGA UA’ kati yao.
Mshindi wa Mechi hii atacheza na Mshindi wa Millwall V Wigan
kwenye Fainal Uwanjani Wembley hapo Mei 11.
Wachambuzi wa Soka huko England wameibatiza Mechi hii ni
Fainali kwani ni imani yao Mshindi wake hawezi kusimamishwa na yeyote kati ya
Wigan au Millwall kwenye Fainali.
0 comments:
Post a Comment