Kocha mkuu wa vinara wa ligi kuu soka nchini Uingereza mashetani wekundu
Manchester United, mscotish Kibabu Alexndar Chapman Ferguson akijulikana kwa
jina la sir Alex Ferguson ameibuka na kujibu mapigo kwa Kocha Roberto Mancini
kuwa mawazo yake kuwa timu za Uingereza zinacheza kwa hofu dhidi ya United
hayana maana yoyote.
Ferguson amesema Mancini anatafuta njia ya kujitetea kutokana na kuweka
rehani ubingwa wake kwani mpaka sasa hana uwezo wa kutetea taji hilo na taarifa
za chini zinaeleza kuwa anaweza kufungashiwa virago baada ya msimu huu
kumalizika.
Ferguson ameongoza kuwa ligi ya Uingereza ni ligi ya ukweli sana kwani mechi zinachezeshwa kihalali na unapopata ushindi unahangaika dakika zote tisini.
Jumatatu ya wiki baaada ya City kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya United katika dimba la united, kocha Roberto Mancini alisema kinachowafanya wapinzania wake kupata mafanikio zaidi msimu huu ni tabia ya timu za ligi hiyo kuiogopa united bila sababu.
Maneno hayo yamemkera kocha Ferguson na leo hii amemshambulia kocha huyo kuwa kwa sasa asahau kutetea taji lake kwa michezo iliyosalia kwani United inajipanga kuendeleza wimbi la ushinidi hapo kesho.
City wameonekana kupoteza mwari safari hii kutokana na kuwa nyuma ya hasimu wake kwa pointi 12 pengo ambalo ni gumu kusawazisha.
United wanaotaka ubingwa wa 20 wa ligi kuu England wanatarajiwa kuongeza pengo hilo dhidi ya City kwani kesho wanasafiri kuwafuata Stoke wakati Mancini atakuwa kibaruani na Vijana wa Rafael Benetez katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la FA.
0 comments:
Post a Comment