Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
Kocha
 wa Real Madrid Mreno Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho bado ana 
imani kubwa kuwa kikosi chake kitabadili kipigo cha mabao 4-1 
walichokipata huko Ujerumani katika mchezo wao wa marudiano dimbani 
Santiago Bernabeu.
“Timu yangu mara siku zote inafanya vitu vya haki, na inaweza kushinda kwa haki katika mchezo wa leo”. Alisema Mourinho leo hii.
Kocha
 huyo aliendelea kusema “Tumekubali kuwa Lewandowski alitufunga mabao 
manne na hatukumfanyia hata faulo mojo. Lakini Dortmund walimfanyia 
Ronaldo madhambi mara tano tangu mchezo kuanza”.
“Unawezaje
 kumaliza dakika 90 bila kumfanyia madhambi mchezaji aliyekufunga mabao 
manne pekee yake, ndio maana nasema timu yangu inacheza kwa haki”. 
Alisisitiza Mourinho.
Leo 
hii Madrid wanaingia uwanjani wakiwa na kibarua kizito cha kupindua 
kipigo cha 4-1 kutoka kwa nyuki wa kaskazini mashariki mwa Ujerumani.
Mabao
 yote ya Dortmund yalitiwa kambani na Robert Lewandowski lakini Mourinho
 alisema timu yake haikumkaba vizuri na ndio maana Mpoland huyo 
hakufanyia madhambi hata kidogo. 
 
Jose
 Mourinho amesema Real Madrid inaweza kuwafunga Dortmund licha ya Robert
 Lewandowski (chini) kuwapa wastani wa mabao matatu yanayotakiwa 
kufungwa na Madrid ili kusonga mbele.
Huyu bwana hakufanyiwa hata rafu mojo ndani ya dakika 90 licha ya kufunga mabao manne pekee yake 
 
Wachezaji wa Real Madrid wakifanya mazoezi kabla ya mchezo wao wa usiku dhidi ya Dortmund uwanja wa Santiago Bernabeu 

 
Sergio Ramos (kushoto) na Xabi Alonso wakipasha misuli yao leo kabla ya mchezo wao wa usiku
DORTMUND
Wakati
 huo huo kocha wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp alisistiza kuwa timu 
yake haitapaniki hata kidogo kupamana na Real Madrid katika uwanja wao 
kwani wanajua watakuwa wanahitaji ushindi kwa nguvu zote.
Flopp aliongeza kuwa ushindi wa 4-1 nyumbani ni mkubwa sana na hadhani kama watakubali kuupoteza leo hii mbele ya Mourinho.
Alipoulizwa kama kama timu yake itashinda mchezo wa leo Flopp alisema “No, sina uhakika lakini nadhani hatuwezi”. 
 
Flopp
 ana uhakika na alisema “Tulicheza na Bayern fainali ya kombe la 
Ujerumani wakati tayari tukiwa mabingwa. Walihitaji sana ushindi 
kufuatia kuwa na msimu mbaya, lakini timu yangu ilitulia na kuwapoteza 
kwa wastani wa maboa 5-2.“Nadhani hata Madrid wataingia na falsafa hii ili kututoa, lakini kama hawa amini hivyo najua watambana sana”. Alisema Flopp. 
 
Klopp na Ilkay Gundogen wakiwa katika mkutano kabla ya mechi dimbani Bernabeu
 
Maandalizi: Dortmund wakifanya mazoezi kabla ya mchezo wao wa leo usiku
Lewandowski
 (kushoto)  ambaye aliwafunga Madrid 4 na mechi iliyopita dhidi ya 
Fortuna Dusseldorf ligi kuu soka nchini Ujerumani “Bundesliga” 
alipumzishwa kwa ajili ya kipute cha leo.
Wakipasha: Marco Reus (kushoto) na Mario Gotze (kulia) wakipiga jalamba

0 comments:
Post a Comment