![]() |
Bondia Athumani Yanga wa timu ya Ashanti Boxing ya Ilala
|
MASHINDANO ya klabu bingwa ya Mkoa wa Temeke yameanza jana jijini, Dar es Salaam huku yakishirikisha timu 20 na yanatarajiwa kufikia tamati Aprili 19 mwaka huu.
Lengo
la mashindano hayo yaliyoanza jana ni kuinua vipaji vya mabondia
chipukizi na kupata vipaji bora watakaokuwa chachu ya maendeleo ya
mchezo nchini.
Kocha
wa kimataifa wa mchezo huo nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ alisema
vijana wanakaoshiriki mashindano hayo walipima uzito katika Ukumbi wa
CCM Kata ya 15, Temeke Dar es Salaam.
Super
D ambaye pia ni kocha wa timu ya Mkoa wa Ilala ambao ni waalikwa katika
michuanohiyo alisema vijana wake kutoka klabu ya Amana na Ashanti
watafanya vema katika mashindano hayo.
Mkoa
wangu umetoa vijana sita ambao naamini watafanya vizuri katika
mashindano hayo kutoa upinzania mkubwa ambao utakuwa chachu ya maendeleo
ya mchezo huo nchini.
Super
D aliwataja baadhi ya mabondia hawo kuwa ni Hussein Mawimbi na Said
Hamisi kutoka klabu ya Amana na Athumani Yanga pamoja na Said Mabunda
kutoka klabu ya Ashanti.
Pia
aliwaomba wadau kujitokeza kusaidia mashindano hayo yanayofanyika
katika ukumbi wa CCM Kata ya 15, Temeke ili kuhakikisha hamasa ya
kuendeleza mchezo huo inapatikana yatakayofanikisha mafanikio ambalo
ndilo lengo kubwa. la mashindano hayo
Kocha
huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo
huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo huo zenye mapambano
makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza
kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama
Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla na Francis Miyeyusho,
Said Mundi na King Class Mawe. na Francis Cheka dhidi ya Japhet Kaseba
mapambano yote mawili mbali na hivyo atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo
wa masumbwi kwa mabondia ambao awana wanaweza kumuona na kujipatia
vifaa mbalimbali
0 comments:
Post a Comment