KLABU
ya Manchester United ya England imeng'olewa kileleni katika orodha ya
jarida la Forbes la klabu tajiri duniani na sasa vigogo wa Hispania,
Real Madrid ndio wanaongoza.
United
imekuwa kileleni tangu wachambuzi wa biashara wa Forbes waanze
kuorodhesha klabu tajiri duniani mwaka 2004, lakini sasa imepigwa bao na
Real.
Barcelona inashika nafasi ya tatu na Arsenal ni ya nne mbele ya Bayern Munich iliyo katika nafasi ya tano.

Wamepitwa: Manchester United wameporomoka nafasi moja katika orodha ya klabu tajiri kwenye jarida la Forbes

Wako juu: Vigogo wa Hispania, Real Madrid wana thamani ya Pauni Bilioni 2.15
Real
ina thamani ya Pauni Bilioni 2.15 (sawa na dola za Kimarekani Bilioni
3.3) - hivyo kuifanya klabu hiyo ya Hispania kuwa chombo cha michezo
chenye thamani kubwa zaidi duniani- na United wana thamani ya Pauni
Bilioni 2.07.

Wamo nne bora: Arsenal wanashika nafasi ya nne nyuma ya Real Madrid, Manchester United na Barcelona
10 BORA YA KLABU TAJIRI DUNIANI ZA FORBES...

0 comments:
Post a Comment