![]()  | 
|   
ALEX MSAMA 
 | 
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI
 ya Msama Promotions inatarajia kufanya uzinduzi mkubwa wa albamu ya 
sita ya Haleluya, ambayo inawahusisha wanamuziki wa Injili wa nchi za 
Afrika Mashariki.
Uzinduzi
 wa albamu hiyo unatarajiwa kufanyika Septemba mosi mwaka huu, ambapo 
kutakuwa na wanamuziki mbalimbali wa muziki wa Injili kutoka ndani na 
nje ya nchi ambao watausindikiza uzinduzi huo.
Akizungumza
 leo hii, Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amebainisha kuwa 
maandalizi ya albamu hiyo yanakwenda vizuri na wanauhakika wa kufanya 
mambo mazuri zaidi.
“Tumeshaanza
 maandalizi ya Haleluya Collections, tumejipanga kutoa albamu bora 
iliyoshiba, itakuwa ni albamu kali ya muziki wa Injili nchini na Afrika 
kwa ujumla,”alisema Msama.
Alieleza kuwa uzinduzi huo utafanyika pia kwenye mikoa zaidi ya saba, ambapo utaratibu wa kuteua mikioa hiyo bado unaendelea.
Alisema uzinduzi huo utakuwa ni wa CD na DVD na albamu hiyo itakuwa imebeba nyimbo zaidi ya tano.


0 comments:
Post a Comment