 >>FENERBAHCE YAICHAPA LAZIO!!
>>FENERBAHCE YAICHAPA LAZIO!! 
MECHI 4 za Robo Fainali za 
EUROPA LIGI zilichezwa jana na England, yenye Timu 3, ilipata matokeo 
tofauti kwa Timu zao Chelsea, Tottenham na Newcastle.
ZIFUATAZO NI TAARIFA KUHUSU MECHI HIZO:
TOTTENHAM 2 FC BASEL 2 
YALE matumaini ya Tottenham kutinga Nusu
 Fainali za EUROPA LIGI jana yaliingia dosari kubwa baada ya kutoka sare
 ya Nyumbani ya Bao 2-2 na Basel ya Uswisi walipolazimika kutoka 2-0 
nyuma na kusawazisha.
Uwanjani White Hart Lane, Basel 
walitangulia kufunga kwa Bao za haraka haraka za Valentin Stocker na 
Fabian Frei lakini Emmanuel Adebayor akaipatia Spurs Bao moja na kufanya
 matokeo kuwa 2-1 hadi Mapumziko.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Tottenham 2
-Adebayor Dakika ya 40
-Sigurdsson 58
Basel 2
-Stocker Dakika ya 30
-Frei 34
 ++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Gylfi Sigurdsson 
aliisawazishia Spurs na kufanya Gemu kuwa 2-2 lakini Spurs walipataka 
pigo kubwa pale Mchezaji wao wa kutegemewa Gareth Bale alipotolewa nje 
kwa Machela baada ya kuumia enka.
Bale ndie Mfungaji Bora wa Tottenham 
akiwa na Mabao 22 Msimu huu na tangu Januari Mosi, Tottenham 
hawajashinda Mechi yeyote ambayo Bale hajafunga.
VIKOSI:
Tottenham: Friedel, Naughton, Gallas, Vertonghen, Assou-Ekotto, Dembele, Parker, Lennon, Bale, Holtby, Adebayor
Akiba: Lloris, Dempsey, Huddlestone, Dawson, Sigurdsson, Livermore, Caulker.
Basel: Sommer, Steinhofer, Schar, Dragovic, Voser, El-Nenny, Die, Salah, Fabian Frei, Stocker, Streller
Akiba: Vailati, Ajeti, David Degen, Alexander Frei, Cabral, Sauro, Zoua.
Refa: Milorad Mazic (Serbia)
CHELSEA 3 RUBIN KAZAN 1
WAKICHEZA kwao Stamford Bridge, Fernando
 Torres aliifungia Chelsea Bao 2 na Victor Moses Bao moja na kuipa 
ushindi Chelsea wa Bao 3-1 dhidi ya Rubin Kazan ya Urusi.
Bao pekee la Rubin Kazan lilifungwa na Bibras Natkho kwa Penati baada ya John Terry kuunawa Mpira.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Benfica 3
-Torres Dakika ya 16 & 70
-Moses 32
Rubin Kazan 1
-Natcho Dakika ya 41 [Penati]
 ++++++++++++++++
Hata hivyo, Chelsea wanajua bado wana 
kibarua kigumu cha kutinga Nusu Fainali katika Mechi ya Marudiano huko 
Moscow Wiki ijayo kwani Rubin Kazan ni wagumu wakiwa kwao na Msimu huu 
kwenye Mashindano haya wameshazitupa Timu ngumu wakiwemo waliokuwa 
Mabingwa Kombe hili Atletico Madrid na nyingine ni Partizan Belgrade, 
Inter Milan na Levante.
VIKOSI:
Chelsea: Cech, Azpilicueta, Terry, Luiz, Bertrand, Ramires, Lampard, Moses, Benayoun, Mata, Torres
Akiba: Turnbull, Ivanovic, Oscar, Mikel, Hazard, Ferreira, Marin.
Rubin Kazan: Ryzhikov, Cesar Navas, Kuzmin, Kaleshin, Ansaldi, Sharonov, Orbaiz, Roman Eremenko, Karadeniz, Natcho, Dyadyun
Akiba: Arlauskis, Ryazantsev, Kasaev, Kisliak, Marcano, Tore, Rondon.
Refa: Gianluca Rocchi (Italy)
BENFICA 3 NEWCASTLE 1
Newcastle, wakicheza ugenini huko 
Estadio da Luz, Mjini Lisbon, Ureno, walijikuta wakisambaratika katika 
Kipindi cha Pili na kutwangwa Bao 3-1 na Benfica.
Papiss Cisse aliwapa matumaini Newcastle
 kwa kufunga Bao la kwanza kabisa baada ya pasi safi ya Moussa Sissoko 
lakini alishindwa kuipa Bao la pili pale shuti lake lilipopiga mwamba na
 mara tu baada ya hapo Rodrigo akaisawazishia Benfica.
++++++++++++++++
MAGOLI:
Benfica 3
-Rodrigo Dakika ya 25
-Lima 65
-Cardozo 70 [Penati]
Newcastle 1
-Papiss Cisse Dakika ya 12
 ++++++++++++++++
Kipindi cha Pili, Cisse tena akapiga 
posti na Benfica wakapiga Bao la pili baada ya kuinasa pasi mbovu ya 
nyuma ya Beki wa Newcastle Davide Santon na Lima kufunga.
Oscar Cardozo aliipa Benfica Bao la Tatu kwa Penati baada ya Steven Taylor kuunawa Mpira.
FENERBAHCE 2 LAZIO 0 
WAKICHEZA kwao, Fenerbahce walitumia 
vizuri mwanya wa kucheza na Mtu 10 Lazio na kufunga Bao za mwishoni na 
kuibuka na ushindi wa Bao 2-0.
Lazio walipata pigo baada ya Ogenyi 
Onazi kupewa Kadi za Njano mbili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu katika 
Dakika ya 47 na upungufu huo uliwasaidia Fenerbahce kushinda Mechi hii.
Katika Dakika ya 79, Pierre Webo 
alifunga kwa Penati kufuatia Stefan Radu kuunawa Mpira na Straika wa 
zamani wa Liverpool, Dirk Kuyt, akafunga Bao la pili baada ya kunasa 
Mpira uliobabatiza Walinzi kufuatia frikiki ya Caner Erkin.
VIKOSI:
Fenerbahce: Demirel; Gonul, Yobo, Korkmaz, Ziegler; Topal, Meireles; Kuyt, Cristian, Sow; Webo
Lazio: Marchetti; Ciani, Cana, Radu, Gonzalez; Candreva, Onazi, Hernanes, Lulic; Ederson; Kozak
EUROPA LIGI:
ROBO FAINALI:
MARUDIANO
11 Aprili 2013
[Saa 1 Usiku]
Rubin Kazan v Chelsea [1-3]
[Saa 4 Dak 5 Usiku]
Newcastle v Benfica [1-3]
Basel v Tottenham [2-2]
Lazio v Fenerbahce [0-2]
NUSU FAINALI
Mechi ya 1=25 Aprili 2013
Mechi ya 2=2 Mei 2013
FAINALI
15 Mei 2013
UWANJA wa AMSTERDAM ARENA
 
0 comments:
Post a Comment