>>WADAI: ‘HAJUI SHERIA ZA GEMU!!!’
 Barcelona
 wamewasilisha malamiko rasmi kwa UEFA kuhusu uchezeshaji wa Refa 
Wolfgang Stark walipotoka sare ya Bao 2-2 na Paris St Germain katika 
Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGIhivi Juzi.
Barcelona
 wamewasilisha malamiko rasmi kwa UEFA kuhusu uchezeshaji wa Refa 
Wolfgang Stark walipotoka sare ya Bao 2-2 na Paris St Germain katika 
Mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGIhivi Juzi.
Barca hawakufurahishwa na uchezeshaji wa
 Stark na wamedai Refa huyo kutoka Germany ‘hajui Sheria za Gemu’ kwa 
kuruhusu Mpira uendelee wakati Wachezaji wawili wa Barca, Javier 
Mascherano na Jordi Alba, walikuwa wamelala chini baada ya kugongana 
wenyewe.
Barca wamedai Refa huyo alipaswa 
kusimamisha Mpira wakati huo na pia hakupaswa kulikubali Bao la kwanza 
la PSG ambalo alifunga Zlatan Ibrahimovic wakati akiwa Ofsaidi.
Msemaji wa Barcelona, Toni Freixa, 
amesema Klabu yao imewaandikia UEFA kufuatia mlolongo wa makosa ya Refa 
huyo ikiwa dhahiri kuwa hakufuata Sheria za Soka.
Uamuzi wa kumshitaki Refa huyo UEFA ulichukuliwa na Barcelona baada ya Bodi ya Klabu hiyo kukutana Siku ya Alhamisi.
Msimu huu, Wadau wengi wamekuwa 
wakilalamika kuhusu uchezeshaji wa Marefa usiokuwa makini hasa baada 
Mchezaji wa Manchester United, Nani, kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu Man 
United walipofungwa 2-1 na Real Madrid lakini tukio kama la Nani 
lilifanywa mara mbili na Wachezaji wa Real Madrid walipoifunga 
Galatasaray Bao 3-0 juzi Jumanne lakini Wachezaji wa Real hawakupewa 
Kadi yeyote.
KUTOKA SOKA IN BONGO 




0 comments:
Post a Comment