Sunday, January 27, 2013


Jerry Tegete akichomoka kushangilia baada ya kuifungia Yanga bao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya TZ Prisons Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni hii. Yanga ilishinda 3-1.


YANGA SC imezidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya jioni hii kuitandika Prisons ya Mbeya mabao 3-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga imetimzia pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa wastani wa pointi tano, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 27 na Simba 26.
Hadi mapumziko, timu hizo zilikuwa tayari zimefungana bao 1-1, Yanga wakitangulia kupata bao lao dakika ya 10 kabla ya Prisons kusawazisha dakika ya 17.
Bao la Yanga lilifungwa na Jerry Tegete aliyeunganisha krosi nzuri ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia, wakati la Prisons lilifungwa na Elias Maguri, aliyeunganisha krosi nzuri ya Misango Magai kutoka wingi ya kushoto.
Tegete akiigusa nembo ya Yanga baada ya kufunga la tatu. PICHA ZAIDI BAADAYE.
Yanga walicheza vizuri dakika 15 za mwanzo na baada ya hapo, timu hizo zilianza kushambuliana kwa zamu, ingawa Watoto wa Jangwani ndio waliopoteza nafasi nzuri zaidi za kufunga.
Kipindi cha pili, Yanga walirudi na kasi nzuri kusaka ushindi na iliwachukua dakika 11 tu kupata bao la pili, lililofungwa na Mbutu Twite baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Prisons.
Wakati Prisons wakiwa kwenye jithada za kusaka bao la kusawazisha, walijikuta wakitandikwa bao la tatu, Tegete tena akiwainua vitini mashabiki wa Yanga, baada ya kupokea pasi nzuri ya Nurdin Bakari dakika ya 65.
Baada ya bao hilo, Yanga walianza kuonyesha vitu vya Uturuki walipoweka kambi ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko huu wa pili wa Ligi Kuu, wakicheza soka ya madoido pasi nyingi, uzungu na kila aina ya mbwembwe, ili mradi tu kuwaburudisha mashabiki wake.
Mapema kabla ya mchezo huo, kiungo wa Yanga, Frank Domayo alipatwa na Malaria ya ghafla na kuenguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake akaanza Nurdin Bakari, wakati mshambuliaji mpya wa Prisons, Emmanuel Gabriel alienguliwa kwenye kikosi cha kwanza na nafasi yake akachukua Elias Maguri, kwa sababu ya kutokuwa na leseni ya TFF ya kumruhusu kucheza Ligi Kuu. Suala la leseni ya Gabriel, dhahiri ni uzembe wa viongozi wa Prisons.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite/Juma Abdul dk 82, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Nurdin Bakari/David Luhende dk 66, Didier Kavumbangu/Hamisi Kiiza dk 64, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.
TZ Prisons; David Abdallah, Aziz Sibo, Henry Mwalugala, Lugano Mwangama, Jumanne Elfadhil, Nurdin Issa, Sino Augustino, Freddy Chudu, Elias Maguri, Misango Magai/John Matei dk58 na Jeremiah Juma. 

FRANK DOMAYO TAABANI, AUGUA GHAFLA NA KUENGULIWA KIKOSINI YANGA LEO

Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akiwa amelala katika zahanati ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mida hii, baada ya kupatwa na Malaria ya ghafla. Domayo ilikuwa aanze mechi ya leo, lakini kutokana na kuugua huko ghafla, sasa nafasi yake ataanza Nurdin Bakari.

Kiungo wa Yanga, Frank Domayo akiwa amelala katika zahanati ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mida hii, baada ya kupatwa na Malaria ya ghafla. Domayo ilikuwa aanze mechi ya leo, lakini kutokana na kuugua huko ghafla, sasa nafasi yake ataanza Nurdin Bakari.

SIMBA NA LYON ZAINGIZA MILIONI 58

Ngassa katikati, kulia Redondo na kushoto Kiemba

Na Boniface Wambura
MECHI namba 92 ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon, imeingiza Sh. 53,756,000.
Watazamaji 9,408 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 12,499,752.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 8,200,067.80.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya Uwanja sh. 6,355,806.33, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 3,813,483.80, Kamati ya Ligi Sh. 3,813,483.80, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh. 1,906,741.90 na Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA) Sh. 1,483,021.48.
Katika mechi hiyo, hadi mapumziko Simba SC walioweka kambi ya wiki mbili Oman kujiandaa na mzunguko huu, tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-0, yaliyotiwa kimiani na Mrisho Khalfan Ngassa mawili dakika za 19 na 39 na Ramadhan Suleiman Chombo ‘Redondo’ dakika ya tatu ya mchezo huo.
Redondo aliifungia Simba SC bao la kwanza dakika ya tatu, akiunganisha krosi nzuri ya Ngassa kutoka wingi ya kushoto na kufumua shuti akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Lyon.
Bao hilo liliwatia chaji Simba SC na kuanza kucheza soka maridadi zaidi, wakionana kwa pasi za mitindo yote, ndefu, fupi, za juu, chini hadi visigino na haikushangaza dakika ya 19 walipopata bao la pili.
Ilikuwa ni kazi nzuri ya Ngassa mwenyewe, ambaye baada ya kupata pasi ya Mwinyi Kazimoto Mwitula aliitoka ngome ya Lyon kabla ya kumchambnua kipa wa timu hiyo, Abdul Seif.
Baada ya kufunga bao hilo, Ngassa alikwenda moja kwa moja kwenye benchi la wachezaji wa akiba na kukumbatiana na Haruna Moshi Shaaban ‘Boban’ kisha kuwapa mikono wachezaji kadhaa na kurejea uwanjani.
Lyon walipoteza nafasi nzuri ya kupata bao dakika ya 31, baada ya Shamte Ally Kilalile kukosa penalti.
Refa Israel Mujuni alitoa penalti hiyo baada ya beki Paul Ngalema kumkwatua beki Fred Lewis aliyepanda kusaidia mashambulizi, hata hivyo mkwaju wa kwanza wa Shamte ulipanguliwa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja, lakini mwamuzi akaamuru irudiwe kwa madai kipa huyo alitokea kabla ya mpira kupigwa na safari hiyo mpigaji akapiga nje kabisa.
Simba iliongeza kasi ya mashambulizi ikitumia mipira ya pembeni, kulia akiteleza Chanongo na kushoto Ngassa, timu ikichezeshwa vyema na viungo watatu katikati, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Jonas Mkude. Ilikuwa burudani kwa mashabiki wa Wekundu hao wa Msimbazi, kwa jinsi ambayo timu yao ilitawala mchezo.
Kazi nzuri ya Chanongo aliyeteleza wingi ya kulia huku akiruka madaluga ya mabeki wa Lyon, iliipatia Simba bao la tatu baada ya krosi yake nzuri kuunganishwa vyema kimiani na Ngassa.  
Baada ya kufunga, Ngassa alishangilia kwa aina yake bao hilo, kwanza akitambaa hadi langoni na kisha kujilaza kwenye nyavu kubwa kama yeye ndio mpira.
Baada ya hapo, aliinuka na moja kwa moja kwenda tena kwenye benchi la wachezaji wa akiba akianza kushangilia na Boban, baadaye wachezaji wengine na kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ambaye alitumia kama sekunde 30 akizungumza naye jambo.  
Kipindi cha pili, Lyon walibadilika na kuwabana Simba SC wasiongeze mabao zaidi, huku wao wakifanikiwa kupata bao la kufutia machozi, lililofungwa na Bright Ike dakika ya 59, pasi ya Fred Lewis.
Dakika ya 64 Ngassa alipoteza nafasi ya kufunga mabao matatu katika mchezo mmoja, baada ya kukosa penalti.
Katika mechi nyingine jana, Mtibwa Sugar ililala 1-0 nyumbani mbele ya Polisi Morogoro, bao pekee la Muzamil Said dakika ya 76,  Coastal Union iliifunga Mgambo JKT 3-1, Ruvu Shooting iliilaza 1-0 JKT Ruvu, bao pekee la Abdulrahman Seif dakika ya 90 Azam FC imeshinda 3-1 dhidi ya Kagera Sugar na JKT Oljoro imeilaza 3-1 Toto Africans.
Ushindi wa Azam ulitokana na mabao ya Abdi Kassim ‘Babbi’ dakika ya 20 na Khamis Mcha dakika za 31 na 66, wakati la Kagera lilifungwa na Paul Ngway dakika ya 82 na sasa timu hiyo imejiimarisha katika nafasi ya pili kwa kutimzia pointi 27, sasa ikizidiwa mbili tu Yanga iliyo kileleni.
Uwanja wa Mkwakwani, Tanga mabao ya Coastal yalifungwa na Philip Mugenzi dakika ya 18, Daniel Lyanga dakika ya 78 na Joseph Mahundi dakika ya 81, wakati la Mgambo lilifungwa na Peter Mwalyanzi dakika ya 89.
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, mabao ya Oljoro yalifungwa na Hassan Isihaka dakika ya 15, Paul Nonga dakika ya 51 na 57, wakati la Toto lilifungwa na Selemani Kibuta dakika ya 73.
Ligi hiyo itaendelea kesho wakati vinara, Yanga SC watakapomenyana na TZ Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video