Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Ndugu Abdurahman Kinana akishuka
kwenye treni mara baada ya kuwasili leo asubuhi kwenye kituo kikuu cha
Reli ya kati cha mjini Kigoma a.k.a (Mwisho wa Reli) akiongozana na
wajumbe wenzake wa Sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM),
Sekretarieti hiyo iliamua kusafiri kwa jia ya Treni kutoka jijini Dar
es salaam mpaka mkoani Kigoma ambako chama cha Mapinduzi kinaadhimisha
miaka yake 36 Februari 3, Mwaka huu, kwenye uwanja wa Lake Tanganyika.
Lakini Pia Kinana amesema hii ni
Kuunga mkono juhudi za Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe na
wafanyakazi wa Shirika la Reli (TRL), kwa kuwa na moyo wa kizalendo na
kuamua kusimama kidete katika kuhakikisha huduma ya chombo hicho muhimu
kwa mikoa ya Magharibi Kinarudi na kuanza kufanya kazi.
Katibu
Mkuu wa CCM ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wananchi
waliojitokeza katika mapokezi mara baada ya kuwasili kwa treni na
wajumbe wa Sekretarieti ya CCM mjini Kogoma leo asubuhi.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdurahman Kinana na ujumbe wajumbe wenzake wakiwa kwenye
kituo kikuu cha reli mkoani Kigoma mara baada ya kupokelewa na wananchi
wakitokea jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya
CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro na Nape Nnauye
Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Itikadi na Uenezi.
PICHA NA FULLSHANGWE BLOG
0 comments:
Post a Comment