
Idadi
 ya wadau waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi katika 
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeongezeka ambapo wengine 
saba wamechukua leo (Januari 15 mwaka huu) na kufanya idadi yao kufikia 
26.
Hata
 hivyo, idadi hiyo ni kwa wale wanaochukua fomu hizo katika ofisi za 
TFF, kwani vilevile zinapatikana kupitia tovuti ya TFF ya www.tff.or.tz ambapo mwisho wa kuchukua na kurejesha ni saa 10 kamili alasiri Januari 18 mwaka huu.
Waliochukua
 leo ni Michael Wambura anayewania umakamu wa rais wakati kwa wajumbe wa
 Kamati ya Utendaji ni Mbasha Matutu, Muhsin Balhabou, Salum Chama, 
Titus Osoro na Zafarani Damoder.
Idadi
 kamili ya waliochukua Michael Wambura, Ramadhan Nassib na Wallace Karia
 (Makamu wa Rais). Kwa upande wa wajumbe na kanda zao kwenye mabano ni 
Salum Chama (Kagera na Geita), Mugisha Galibona, Samuel Nyalla, Titus 
Osoro na Vedastus Lufano (Mara na Mwanza).
Epaphra
 Swai na Mbasha Matutu (Shinyanga na Simiyu), Charles Mugondo, Elly 
Mbise na Twahili Njoki (Arusha na Manyara), Yusuph Kitumbo (Kigoma na 
Tabora), Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja na Selemani Kameya (Katavi 
na Rukwa) na James Mhagama (Njombe na Ruvuma).
Athuman
 Kambi (Lindi na Mtwara), Hussein Mwamba na Stewart Masima (Dodoma na 
Singida), Farid Nahdi (Morogoro na Pwani), Khalid Mohamed (Kilimanjaro 
na Tanga) na Muhsin Balhabou, Shaffih Dauda na Zafarani Damoder (Dar es 
Salaam).
Naye Said Mohamed amechukua fomu ya kuwania umakamu mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
UCHAGUZI TAIFA KUFANYIKA DAR ES SALAAM
Uchaguzi
 wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) 
utafanyika Jumamosi (Januari 19 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa 
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Kwa
 mujibu wa Katibu Mkuu wa TAFCA, Eugene Mwasamaki, mikoa ambayo tayari 
imefanya uchaguzi wa viongozi inatakiwa kuwasilisha muhtasari wa mkutano
 uliowaingiza madarakani. Muhtasari huo uwasilishwe TAFCA kabla ya 
keshokutwa (Januari 17 mwaka huu).
| Eugene Mwasamaki | 
Mkoa
 utakaoshindwa kutuma muhtasari ndani ya muda uliotolewa utakosa haki ya
 kushiriki katika uchaguzi huo uliovutia wagombea watano. Wagombea hao 
ni Oscar Korosso (Mwenyekiti), Lister Manyara (Makamu Mwenyekiti), 
Michael Bundala (Katibu Mkuu) na Magoma Rugora na Wilfred Kidao 
wanaowania ujumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu 
Tanzania (TFF).

0 comments:
Post a Comment