Sunday, January 6, 2013


Januari 7, si kesho???? au kalenda yangu bado imelala au macho yango bado yapo Analojia

Ni siku ya kipekee kwenye viunga vya jiji la Zurich Usiwsi ambapo mchezaji bora mwaka msimu wa 2011/12 atajulikana kwa kukata mzizi wa fitina na kumaliza ubishi wa nani mkali baina ya Lionel Messi, Andres Iniesta na Cristiano Ronaldo.


Lakini nini wasemacho wataalam na waasisi wa soka duniani? Tovuti ya Fifa.com juzi ilikusanya mawazo ya wanandinga maarufu na wachambuzi pamoja na makocha mbalimbali ili kuzungumzia mchezaji anayefaa kutwaa 'mwali huyo'


KUHUSU CRISTIANO DOS SANTOS ALVEROA RONALDO........


>> "Ureno ina timu ya taifa iitwayo Cristiano Ronaldo! na kikundi cha wachezaji hupenda kuikimbilia timu hiyo." Carlos Queiroz.



>> "Cristiano ni tukio 'phenomenon'. Aina ya uchezaji wake ni wa kipekee. Ni aian aya mchezaji amabye kila sikku hupenda kuona ana 'pafomu' zaidi ya jana. Ana hamu na uwezo wa kufunga mabao an kuwahimiza wachezaji wawapo kwenye vyumba vya kubadilisha nguo. Ni mshambuliaji wa aina yake kuwahi kuvaa uzi wa Madrid.” Emilio Butragueno


>> "Ni mchezaji asiyeaminika. Tumekuwa na wachezaji muhimu na wakali na Ronaldo kiukweli ni mmoja wapo. Ingawaje ana kipaji asilia, lakini amekuwa akijiimarisha zaidi, anpiga tizi haswa. Alikuwa wa thamani kubwa kwa Madrid.”

Sir Alex Ferguson.


Cristiano Dos Santos Ronaldo- Ureno na Real Madrid

>> "Suala lililomtokea Ronaldo, pia lilimkuta Beckham – watu wamekuwa wakiwakosoa sababu ya mvuto wao. Lakini kwangu mimi mchezaji ni Ronaldo . U kasi, mrefu, ni mzuri kwa mipira ya vichwa , kiufundi ni mzuri, kupiga penaliti friki kick na ni kiongozi pia. Nafikiri Cristiano Ronaldo ndiye pekee .” Ruud Gullit


>> “Cristiano Ronaldo amekuwa akipigana katika suala la kiwango cha kimataifa kwa miaka mingi. Wachezaji bora sanjari na Lionel Messi, Ronaldo alionekana akijituma sana, akipigana vilivyo akiwa na timu ya Ureno. Lakini baada ya kupata mechi nyingi za mara kwa mara, Ronaldo alianza kufunga mabao matatu na kuiaidia Ureno kutinga nusu fainalipasipo kutarajia. Alionesha watu wa nchini mwao kuwa anafaa pale Lisbon.”

Diego Maradona wakati wa michuano ya EURO 2012

>> “Messi ni mchezaji bora lakini Cristiano ni janga jingine. Ni mchezji wa juu Duniani kwa sasa sababu ana kila sababu ya kuitwa hivyo. Ni mwepesi, mwenye nguvu , anafunga, ana kiwango cha kusaidia timukupata ilichohitaji. Sijawahi kuona mchezaji mwenye kipaji kama hicho. Mpira umebadilika sana, ana ninafiki kuwa wachezaji kama Pele, Di Stefano na Maradona walitakuwa kufanya kama Cristiano anachifanya kwa sasa kwa ubora wake.” Nuno




KUHUSU ANDRES INIESTA RUJAN...........



>> “Hakika ni Andres Iniesta. Sio kusema ni kucheza vema na kupata kombe pale Barcelona, lakini pia upande wa timu ya taifa ambapo unangalia kiwango cha mchezaji kama ni cha ukweli. Hilo ndilo lililotatiza enzi za kina Pele, Diego Maradona na Zinedine Zidane. Akiwa na Spain, Iniesta ameonesha kuwa ni mmoja wa wachezaji bora kuwahi kutokea na ndiyo maana namchukulia zaidi ya Messi au Ronaldo. Licha ya kwamba hawa watu wawili (Messi na Ronaldo) wana hadhi ya upachikaji mabao kwa klabu zao lakini hawajashinda lolote wakina na timu za taifa.” Boris Becker



>> “Kwenye mkutano na wandishi wa habari wamekuwa wakiniuliza mara kwa mara swali hilo kama ni Messi au Ronaldo kuwa bora, lakini kwangu ipo wazi: Andres Iniesta ni nmaba moja. Anaweza kufanya kitu lolote atakalo akiwa uwanjani.” David Silva



Andrea Lujan Iniesta - Hispania na Barcelona


>> "Hakua mengi ya kuongelea juu ya Iniesta kama ilivyo kwa Messi, lakini napenda kuona akitwaa medsli ya Ballon d'Or. Inamfaa kwa wasifu wake akiwa na Barcelona pamoja na Hispania. Amefanya kila jema anaweza kutengeneza nafasi, kufunga kama wengien wafanyavyo. Iniesta ni wa maajabu ambaye hujua lipi la kufanyaakiwa na mpira .” Luis Fernandez


>> “Ni mtu mwenye upeo wa juu sana. Anahimiza nidhamu uwanjani. Kama mpenda mpira nijivunia kuwa nimecheza naye. Anafanya tofauti na kufanya vitu ambavyo si kila mmoaj anaweza kufanya." Sergio Ramos


"Ni mwangalia Iniesta na niligundua kuwa, hata katika umri wangu, ningekuwa najifunza vitu vipya kutoka kwake." Juan Roman Riquelme katika miaka yake sita abaada ya kuacha soka.


>> “Akiwa na mpira, ni kama kila kitu kimesimama– kama vile Kamera zinakwenda 'slow motion'. “Nimekuwa nikicheza naye tangu tukiwa na miaka 15, na sikuwahi kuona akicheza vibaya.” Fernando Torres



KUHUSU LIONEL MESSI ANDREW GEORGE........



>> "Huwezi kumlinganisha yeyote na Messi. Cristiano Ronaldo ni mtu mkubwa katika mpira lakini Messi ni wa kutoka sayari nyingine. Anaweza kukimbia kasi akiwa na mpiara zaidi ya hata akiwa bila kitu. Ni kama vile anacheza aina nyingine ya mchezo. Ni vigumu kufanya vitu avifanyavyo yeye." Alfio Basile


>> "Rekodi yangu ilikaa kwa miaka 40 – mabao 85 katika mechi 60 games – na sasa mchezaji bora wa dunia ameivunja. Nimempogeza kwa hilo. Ni mchezaji mzuri na wa kiwango cha kisasa ana nina dhani anaweza kupata mbao moja ana mawili zaidi ya haya katika 2012 na tena anaweza akashikiria rekodi yake kwa miaka 40 mingine. Ni wa ajabu sana!" Gerd Muller kuhusu Lionel Messi baada ya kuvunja rekodi ya dunia ya kufunga mabao mengi ndani ya mwaka mmoja 2012 huku yeye akimaliza mwaka na mabao 92!



>> "Baadhi ya watu hawampendi Ronaldo sababu ni mchezaji bora, mwenye mtazamo na mvuto wa kimapenzi kwa wasichana wote, Watu hupata wivu kwa hilo. Kitu kimoja kibaya katika maisha ya Ronaldo ni Messi !!. Kama asingekuwa yeye, Ronaldo angekuwa mchezaji bora duaniani kwa miaka 5 mpaka sasa." Luiz Felipe Scolari.



>> “Akademi ya Ufalme ya Hispania inahitaji kuja na neno jipya litakalo eleza hasa nini Messi anachofanya uwanjani.” Alejandro Sabella, aliitaka Organization inayoshughulikia lugha ya Kihispania kutafuta neno jipya la kueleza namba No10 ya Muargentina huyo akiwa uwanjani.



Lionel Andrew Messi- Argentina na Barcelona


>> "Messi ni Mungu!!– kama mwanadamu na pia kama mchezaji. Ni matumani yangu kuwa atashinda kombe la sunia akiwa na Argentina. Kwa Mungu wa duniani, wote nawambia kwamba mpe nafasi uone.” Samuel Eto'o


>> “Kama Michael Jordan katika kikapu, Messi amelimiliki soka. Watu wachache katika historia wameteka michezo yao kama Jordan na Messi walivyofanya. Nawapa pole kwa wale wanaotaka kushindana na Messi katika mataji– haiwezekani , huyu kinda ni kipekee dunia hii. Hafungi mabao basi tu, ila hufunga mabao yenye umuhimu na kiani na kila moja huwa zuri zaidi ya linalopita.” Pep Guardiola kocha wa zamani wa Barcelona.


Blogs mbalimbali zimekuwa zikiendesha mjadala kuhusu nani kuibuka mchezaji bora na kesho kupitia Supersport , matangazo yatarushwa moja kwa moja kutoka Zurich Uswisi na mbivu ama mbichi zitajulikana


KESHENI MKIOMBA

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video