Imeelezwa kuwa huduma za usafiri wa anga
zinahitajika zaidi kutokana na kipato cha wananchi wengi kuwa cha chini kwa
kuwa gharama za maisha zinazidi kuongezeka.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa baraza la kutetea
haki za watumiaji wa usafiri wa Anga Juma Fimbo wakati akielezea namna
walivyopokea punguzo la nauli kutoka kampuni ya ndege ya Fast Jet.
Mwenyekiti huyo amesema utaratibu wa kutoa ofa ya
punguzo la bei kwa abiria lipo ulimwenguni kote ili kuwasaidia walaji kupata
usafiri kwa bei nafuu lakini wenye masharti ya kupunguza baadhi ya vitu.
Bwana Fimbo amesema hawajapokea malalamiko kutoka
kwa watumiaji kudaiwa kutapeliwa na kampuni ya Fast Jet kwani kama kuna malalamiko
wanatakiwa kuyawasilisha rasmi kwa maandishi.
Amesema kutokana na mfumo wa uchumi huria imekuwa
vigumu kwa serikali kupunguza gharama za usafiri kupitia kodi za wananchi kama
ilivyowahi kutokea miaka ya nyuma wakati shirika la ndege Tanzania likifanya
kazi kwa ufanisi.

0 comments:
Post a Comment