Wednesday, January 2, 2013



Watanzania wametakiwa kuacha mawazo potofu juu ya mgawanyo wa rasilimali zilipo nchini kwa sababu zinatumika kwa ajili ya wananchi wote pasipo upendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Mhongo wakati akitoa ufafanuzi kufuatia maandamano ya wananchi mkoani Mtwara kudai gesi inayochimbwa mkoani humo kutowanufaisha. 
Profesa Sospeter Mhongo

Profesa Mhongo amesema maandamano kama hayo yanaweza kuligawa taifa kwa sababu kila mkoa unatoa rasilimali zake ambazo zinatumika na wananchi wa mikoa yote  bila kujali ukanda wa mikoa husika.

Waziri huyo amesema endapo wananchi  wa kila mkoa wataandamana ni hatari kwa amani, utulivu na ustawi wa taifa.

Amewataka wanasiasa kuangalia maslahi ya kiuchumi kwa Taifa badala ya kuwapotosha wananchi na kusababisha mivutano  isiyokuwa ya lazima katika jamii.
Profesa Mhongo amesema serikali inaamini ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Mnazi Bay mpaka jijini Dar es Salaam utalinufaisha zaidi taifa kwa kutumiwa katika viwanda,taasisi na matumizi ya kawaida ya majumbani.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video