WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Mwaka 2012 ya Mkoa wa
Katavi katika vipengele viwili vya Utawala Bora na Uhamasishaji wa ufugaji
nyuki.
Waziri Mkuu alipokea tuzo hizo, kwenye hafla ya kuuaga
mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya
Maji mjini Mpanda,
![]() |
MH.MIZENGO PINDA |
Akitoa maelezo ya utangulizi kabla ya kutangaza majina ya
watunukiwa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Emmanuel Kalobelo alisema
mkoa wa Katavi umeamua kuanzisha mfumo wa utoaji wa Tuzo ya Mkoa kwa lengo la
kuwatambua, kuwatia moyo na kuwapa motisha wananchi na watumishi wa umma
waliofanya vizuri katika nyanja mbalimbali za utoaji wa huduma kwa wananchi.
Sekta zilizopewa tuzo
ni mapato na kodi za Serikali, utawala bora, uchumi na maendeleo, Ulinzi na
usalama, mipango miji, mawasiliano na teknolojia, ufugaji nyuki na hifadhi ya
mazingira, elimu, kilimo na mifugo, michezo, usafirishaji na huduma za jamii.
Waziri Mkuu Mizengo
Pinda anatunukiwa tuzo ya utawala bora, siasa safi na ushiriki katika shughuli
za maendeleo ya wananchi wa jimbo lake la Katavi na Ukanda wa Ziwa Tanganyika
kikamilifu.
Mhandisi Kalobelo amesema Tuzo hiyo itaendelea kutolewa kila mwisho wa mwaka
ambapo wameamu kufanya hivyo ili kuamsha
ari kwa wengine kufanya vizuri zaidi mwaka unaofuata.
0 comments:
Post a Comment